Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
2 Aprili 2026, 15:48:01
Siku 14 baada ya kumaliza hedhi ni siku ya hatari ya kupata ujauzito?
Ndiyo, siku 14 baada ya siku ya mwisho ya hedhi yako inaweza kuwa karibu na siku zako za hatari, hasa kama mzunguko wako wa hedhi ni wa kawaida wa siku 28. Katika mzunguko wa kawaida:
Uovuleshaji hutokea karibu na siku ya 14,
Siku za hatari za kupata ujauzito huanzia takriban siku ya 11 hadi siku ya 17.
Kwa hiyo, ikiwa unashiriki tendo la ndoa katika kipindi hiki, kuna uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito.
Ushauri:
Kujua mzunguko wako wa hedhi ni muhimu ili kubaini siku zako za hatari,
Ikiwa unataka kupata ujauzito, shiriki mapenzi siku za hatari,
Ikiwa unataka kuepuka ujauzito, tumia njia za uzazi wa mpango katika siku hizi.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 14:07:10
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
