top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Charles W, M.D

2 Aprili 2026, 16:17:50

Syndrome ya Asherman

Asilimia 30 ya wanawake wanaokwanguliwa kizazi ili kutoa mimba yenye miezi mitatu au zaidi, hupata makovu makali ndani ya kizazi yanayosababisha ‘Syndrome ya Asherman’. Watu wenye syndrome hii hupata matatizo ya uzazi kama maumivu makali ya hedhi, kutokuona hedhi, ugumba n.k. Tumia njia za uzazi wa mpango, epuka kupata au kutoa mimba zisizotarajiwa.


Syndrome ya Asherman Hutokeaje?


Syndrome ya Asherman hutokea pale endapo kumetokea majeraha kwenye ukuta wa endometria , ukuta wa ndani ya kizazi ambao huhusika katika kushikilia kijusi mara baada ya kuchavushwa. Majeraha huamsha chembe za mwili zinazosababisha michomo kutokea kwenye ukuta huu kisha kupona kwa kuleta makovu.


Visababishi vya Syndrome ya Asherman


Nini kisabababisha syndrome ya Asherman?


  • Makovu ndani ya ukuta wa mji wa mimba kutokana na kukwanguliwa uzazi

  • Makovu ya upasuaji wa kujifungua au kutoa uvimbe wa fibroid ndani ya kizazi

  • Ugonjwa wa Endometriosis

  • Maambukizi ndani ya mfuko wa kiazi kama Kifua kikuu na Kichocho

  • Matibabu ya mionzi


Dalili za syndrome ya Asherman


  • Kupata hedhi nyepesi na kidogo sana

  • Kutokupata hedhi kabisa

  • Kupata maumivu makali ya hedhi licha ya kutokutoka damu

  • Kutoshika ujauzito


Kujiepusha na Syndrome ya Asherman


Endapo unataka kuepuka kupata syndrome ya Asherman, jikinge kupata mimba zisizotarajiwa kwa kutumia njia za uzazi wa mpango


Unaweza kupata taarifa hii sehemu gani?


Soma zaidi kuhusu visababishi, dalili na tiba kwenye makala ya syndromu ya asherman ndani ya tovuti hii.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 16:17:50

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

bottom of page