top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

26 Februari 2021 13:43:56

Kuhama kwa koo

Kuhama kwa koo

Kuhama koo kwenye sehemu yake ya awali hutokana na shinikizo ndani ya kifua karibu na mrija wa trakea.


Kuhama kwa koo inahusishwa sana na tatizo la kitiba linalofahamika kama ‘traumatic pneumothorax’, huku ni kujaa hewa ndani ya kifua kutokana na kupata tundu kwenye kuta za kifua wakati umechomwa na kitu chenye ncha kali kifuani.


Matatizo mengine pia yanaweza kusababisha kuhama kwa koo kama vile endapo yakitokea karibu na mrija wa trakea ni


  • Upasuaji mfano ‘pneumonektomi’

  • Ugonjwa wa kusinyaa kwamapafu atelektasis,

  • Kujaa kwa maji, usaha au damu kwenye chemba ya pleura

  • Saratani ndani ya kifua


Visababishi


  • Kuvimba kwa tezi shingo. Tezi hii kwa vile ipo karibu na koo, hivyo ikiwa inakua, inaweza kusukuma koo upande mmoja.

  • Lymphoma katikati ya kifua- Lymphoma zinazotokea katikati karibu na bomba la koo linalopitisha hewa kuingia kwenye mapafu, hupelekea kuhama kwa koo kutokana na kuweka mgandamizo. Lymhpoma hutokea kwenye tezi limfu ambazo ziko karibu na koo la kila mtu.


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

7 Februari 2022 19:36:19

Rejea za mada hii

bottom of page