Imeandikwa na ULY CLINIC
26 Februari 2021, 14:21:32
Kuona madoa doa au kuona uzi

Ni hali ya macho kuona madoa madoa meusi au ya kijivu, kuona nyuzi ambazo ambazo hupotea ghafla mara unapoamua kuangalia ni nini unachokiona.
Matatizo mengi ya kuona madoa au uzi hutokea kutokana na uzee. Jinsi mtu anavyozeeka, majimaji yaliyo ndai ya jicho yenye jina la vitreous humor hupoteza uzito wake na kuwa majimaji mepesi pamoja kutengeneza madoa madogo sana ambayo huonwa na lenzi ya macho yako kama madoa au nyuzi ndogo.
Dalili hii pia inaweza kumaanisha kuwa kuna tatizo katika misuli ya macho, neva au sehemu inayo husiana na kuona katika ubongo .Tatizo hili linaweza kurekebishwa kwa miwani maalumu au upasuaji.
Visababishi
Husababishwa na mabadiliko ya macho yanayo sabababishwa na umri unapozeeka
Kuvimba nyuma ya jicho
Kuvilia kwa damu machoni
Upasuaji wa macho na matumizi ya baadhi ya dawa za macho
Majeraha kwenye macho (likiwa jicho limepigwa na kitu au kuharibiwa wakati wa ajali)
Ugonjwa wa kisukari unaweza kuharibu mishipa ya damu
Matatizo ya ubongo au macho kushindwa kuratibu uona kwa usahihi
Tatizo la kurithi au kuzaliwa nalo
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:34:26
Rejea za mada hii
1.Luo J, An X, Kuang Y. Efficacy and safety of yttrium-aluminium garnet (YAG) laser vitreolysis for vitreous floaters. J Int Med Res. 2018 Nov;46(11):4465-4471. [PMC free article] [PubMed]
2.Chong SY, Fhun LC, Tai E, Chong MF, Sonny Teo KS. Posterior Vitreous Detachment Precipitated by Yoga. Cureus. 2018 Jan 24;10(1):e2109. [PMC free article] [PubMed]
3.Singh IP. Novel OCT Application and Optimized YAG Laser Enable Visualization and Treatment of Mid- to Posterior Vitreous Floaters. Ophthalmic Surg Lasers Imaging Retina. 2018 Oct 01;49(10):806-811. [PubMed]