Imeandikwa na ULY CLINIC
1 Machi 2021 09:16:10
Kupoteza uwezo wa kutamka maneno
Disarthria ni hali ya kushindwa kutamka vema maneno, hali hii huambatana na kutamka maneno taratibu na kwa tabu bila mpangilio unaotakiwa.
Pia huweza kuambatana na utumiaji wa sauti kutoka puani endapo kisababishi ni tatizo kwenye ukuta wa palate. Mara nyingi inaweza kuchanganywa na neon aphasia, ambapo mtu anapoteza uwezo wa kuongea au kutengeneza maneno.
Dysarthria hutokana na kuharibiwa kwa sehemu ya shina la ugondo inayopelekea kuleta udhaifu kwenye mishipa ya neva ya cranial namba IX, X na XII inayohusika kuongoza kiboksi cha kutengeneza sauti.
Visababishi
Kuisha kwa cerebella kutokana na matumizi sugu ya pombe
Kutojitosheleza kwa mshipa wa damu wa basilar
Botulism
Majeraha ya kichwani
Kunywa sumu ya mercury
Ugonjwa wa multiple sclerosis
Ugonjwa wa Parkinson’s
Ugonjwa wa myasthenia gravis
Kiharusi kwenye ubongo wa kati na shina la ubongo
Kuzidisha dozi ya dawa za kutibu au kuzuia degedege
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022 19:30:48
Rejea za mada hii