Imeandikwa na ULY CLINIC
26 Februari 2021, 14:59:50
Kupungua uzito
Neno kupungua uzito humaanisha hali ya kupungua kwa kiwango cha mafuta yaliyohifadhiwa chini ya ngozi.
Mara chache huweza kuchangiwa na kupungua kwa kiwango cha nyama, maji na madini mbalimbali mwilini. Kupungua uzito kunaweza kuwa kwa kukusudia kama vile kwa kufanya mazoezi, kujinyima kula au bila kukusudia, na hii huweza kuwa dhihirisho la ugonjwa Fulani unaoendelea ndani ya mwili.
Dalili zinazoweza kuambatana na kupungua uzito ni pamoja na kupoteza hamu ya kula uchovu au udhaifu wa mwili.
Kupunguza uzito ni kawaida baada ya ujauzito au kujifungua
Maambukizi ya virusi kama vile VVU
Matumizi ya baadhi ya dawa
Kuwa na saratani
Ugonjwa wa kisukari
Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
Upungufu wa vyakula vya mafuta, wanga na protini
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:32:13
Rejea za mada hii