Imeandikwa na ULY CLINIC
25 Machi 2021, 11:45:05
Kutoisha kwa mkojo baada ya kukojoa
Katika tiba kutoisha kwa mkojo mara baada ya kukojoa hufahamika kama 'urinary tenesmus' na neno 'kutomaliza kukojoa'.
Dalili gani hupata wagonjwa?
Wagonjwa wengi wenye tatizo hili hulalamika kwamba mkojo hauushi wanapokuwa wanakojoa au kuhisi hiamu ya kukojoa muda mfupi tu baada ya kukojoa
Kuna hali na magonjwa mbalimbali ya kitiba yanaweza kusababisha kutokea kwa hisia hizi. Kwa maelezo zaidi soma kuhusu kisababishi kinachoendana kusababisha tatizo lako.
Maambukizi njia ya mkojo- UTI
Mfumo wa mkojo huundwa na figo, njia ya mkojo inayotoka kwenye figo hadi kwenye kibofu (yureta), kibofu cha mkojo na njia ya mkojo inayotoka kwenye kibofu hadi nje ya mwili(yurethra). Maambukizi ya bakteria huweza kuathiri sehemu yoyote ya mfumo huu. Maambukizi kwenye njia hizi husababisha mtu apate hamu ya kukojoa mara kwa mara
Saratani ya tezi dume
Kwa kawaida chembechembe za mwili huzaliwa na kufa kila siku, hii hutokana na asili ya binadamu na kuna seli ambazo zinafanya kazi ya kuharibu chembe ambazo zimezeeka. Endapo chembechembe zinazounda tezi za prostate hazifu na zimekuwa na tabia tofauti au kutofanana na chembe asilia, hii husababisha kutokea kwa saratani ya tezi dume inayopelekea kugandamizi mrija wa urethra na kuleta dalili ya hamu ya kukojoa mara kwa mara.
Saratani ya Kibofu cha mkojo
Endapo saratani ya kibofu cha mkojo ipo, mtu hupata dalili mbalimbali ikiwa pamoja na hisia za kutaka kwenda kukojoa kwa shuruti. Dalili zingine zinaweza kutokea, ni muhimu kusoma kuhusu dalili zingine au kuwasiliana na daktari wako kabla ya kusema kuwa una saratani.
Mawe kwenye figo
Mawe kwenye figo hutengenezea na chumvichumvi zinazotokana na mkojo. Kuna dalili zingine nyingi zinaweza kuambtana na mawe kwenye figo kama vile maumivu makali upande mmoja wa figo yanayosambaa kuelekea kwenye mrija wa mkojo, pamoja na kutoa mkojo weusi. Kusoma dalili zingine zaidi ingia kwenye makala husika shemu nyingine katika tovuti hii
Magonjwa ya zinaa
Ni magonjwa yanayo ambukizwa kwa njia ya kujamiana kama, mfano wake ni kisonono na kaswende. magonjwa mengi ya zinaa hupelekea kupata mkojo mchafu na wakati mwignine mkojo wenye usaha
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:25:47
Rejea za mada hii
1. Raymond T Foster Sir Obstetrics and gynecology clinics of North America 35(2), 235-248, 2008
2. Differential diagnosis of urinary tenses in the dog Stone hewer in practice 19(3), 134-143, 1997