Imeandikwa na ULY CLINIC
25 Machi 2021 12:39:30
Kutokwa na damu ukeni kwenye komahedhi
Kutokwa na damu baada ya komahedhi ni dalili ya kutokwa damu ukeni miezi sita au zaidi baada ya kuingia kwenye koma hedhi.
Wanawake wengi huingia kipinid cha hedhi kukoma baada ya kufikisha umri wa miaka 45.
Kutokwa na damu ukeni baada ya koma hedhi ni ishara kubwa ya kuwa na saratani katika mfumo wa uzazi. Kuna mambo mengine yanayoweza kusababisha kutokwa na damu ukeni baada ya koma hedhi kama vile, maambukizi kwenye njia ya uzazi, kutumia homon za estrogen na kusinyaa kwa uke. Kutokwa na damu ukeni inaweza maanisha pia kuna shida kwenye uke, shingo ya kizazi, au ndani ya mfuko wa kizazi, ovari, mirija ya mayai.
Damu inayotoka huwa na sifa ya rangi ya kahawia, au nyekundu na huweza kuwa matonetone au damu nyingi. Hata hivyo baadhi ya wagonjwa wanaweza kupata damu wanapokuwa wanajisafisha ndani ya uke au wanapokuwa wanashiriki tendo la ndoa. Wanawake wengi haswa wale ambao walikuwa wana hedhi ya damu nyingi, wanaooona dalili hii hupuuzia na hivyo kuchelewa fika hospitali. Unapopatwa na dalili hii ni vema ukafika hospitali karibu nawe kwa uchunguzi na tiba.
Visababishio
Kusinyaa kwa uke
Wanawake walio koma hedhi wanaposhiriki tendo la ndoa au kujisafisa kwa kuingiza kitu ukeni, hupata damu kwa sababu ya michubuko inayotokea ukeni. Michubuko hutokea kirahisi kwa sababu kuta za uke huwa zimesinyaa na pia kwa sababu ya uzalishaji kiUkavu ukeni husababishwa kufuatia ukavu wa uke unaotokea kwenye koma hedhi. Ni vema kuwasilianana daktari upate ushauri na tiba ya tatizo hili endapo linakusumbua. Sifa za kusinyaa kwa uke ni pamoja na kuwa na uke mkavu, kutoa majimaji meupe yanayoweza kuambatana na muwasho, maumivu wakati wa kujamiana na hisia za kuungua ukeni, kusinyaa kwa kinembe, mashavu ya uke na kutokwa na matone ya damu pia huweza tokea.
Saratani ya shingo ya kizazi
Hatua za awali za saratani ya shingo ya kizazi husababisha kutokwa na matone ya damu ukeni au kumwagika kwa damu nyingi ukeni. Mara nyingi damu ukeni hutoka baada ya kushiriki ngono au kujisafisha kwa kuingiza kitu ukeni au wakati mwingine hutoka zenyewe bila sababu. Damu inayotoka huwa na sifa ya kuwa na rangi ya pinki na inayonuka na pia kuwa na maumivu wakati wa kushiriki ngono. saratani inaposambaa sehemu zingine za mwili inaweza kuleta dalili zingine kama vile maumivu ya sayatika, maumivu ya mguu na kuvimba kwa mguu, kupoteza uzito, kukojoa damu, maumivu wakati w akukojoa, kutokwa na damu njia ya haja kubwa na kupooza sehemu ya chini ya mwili.
Polipsi kwenye shingo ya kizazi au ndani ya kuta za uzazi (endometria)
Hii ni uvimbe mdogo kama vidole unaoota kwenye mlango wa shingo ya kizazi au ndani ya kuta ya uzazi. Vimbe hizi zinaweza kusababisha damu kutoka na huwa na rangi ya pinki, yenye makamasi,na hutoka wakati wa kujisafisha au kushiriki ngono au kukenya wakati wa kutoa haja kubwa. Wagonjwa wengi wenye polipsi ndani ya mfuko wa kizazi huwa hawana dalili, hata hivyo wagonjwa wenye
Saratani ya ovari
Saratani ya ovari huzalisha homoni estrogen, homoni hii huamsha kuta za uzazi zijengwe na hivyok kufanya zibomoke kila mwezi na kuleta dalili ya kutokwa na damu. Kutokwa na damu kutokana na saratani hii, mara zote huwa haiambatani na dalili ya kutokwa samu wakati wa kujisafisha au wakati wa kujamiana. Endapo mwanamke atachunguzwa, kutaonekana kuwepo kwa uvimbe eneo la upande mmoja wa mwili, yaani kushoto au kulia ndani ya nyonga kwa uvimbe mkubwa. Uvimbe mdogo mara nyingi si rahisi kutambiliwa hata hivyo vipimo vinaweza kuonyesha.
Saratani ya uke
Kabla ya kutokwa na damu, saratani hii hutanguliwa na dalili ya kupata majimaji ukeni. Kutokwa damu ukeni huweza kutokea bila kuamshwa au kuamshwa kwa kujamiana au wakati wa kujisafisha kwa kuingiza kitu ukeni. Dalili zingine zinaweza kuwa kuwa na kidonda kigumu ukeni, maumivu wakati wa kujamiana, kukojoa mara kwa mara, maumivu ya kibofu cha mkojo na ndani ya nyonga, ndani ya kifuko cha kutunza haja kubwa au kutokwa na damu njia ya haja kubwa pamoja na kupata majeraha maeneo ya nje ya uke.
Matumizi ya dawa
Baadhi ya dawa zinapotumika kwenye kipindi cha komahedhi huweza pelekea kutokwa na damu ukeni baada ya komahedhi. Dawa nyingi zinazosababisha kutokwa na damu ni zile za hormonal Replacement therapy ambazo zina mchanganyiko wa estrogen tu. Mara nyingi shida hii huwa haionekani kwa wanawake wanaotumia homon mchanganyiko wa estrogen na progesterone.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022 19:24:02
Rejea za mada hii
1.The woman with postmenopausal bleeding,Alison H Brand,Australian family physician 36(3),116,200
2.-How should we investigate women with postmenopausal bleeding? Janeth Kumar Gupta, Sheena Wilson,Pershant Desai, Cathy Hau ,Acta obstetricia et gynecologica scandinava 75(5),475-479, 1996
3.Histopathological fingings in women with pastmenopausal bleeding,Thomas Gredmark , Sonja Kvint, Guillaume Havel, Lars-Ake ,Mattson-BJOG: An International Journal of Obstetrics &Gynaecology 102(2), 133-136,1995