Imeandikwa na ULY CLINIC
25 Machi 2021 10:09:51
Mkojo mchafu
Mkojo mchafu imetumika kumaanisha neno tiba la 'urine Cloudiness'. Hii ni hali inayotokea endapo mkojo unatoka ukiwa na uchafu au ukiwa mzito na wenye uchafu mweupe tofauti na kawaida. Mkojo mchafu katika makala hii haimaanishi kukojoa mkojo wenye rangi ya njano.
Visababishi
Maambukizi ya njia ya mkojo-UTI
Mfumo wa mkojo huundwa na figo, njia ya mkojo inayotoka kwenye figo hadi kwenye kibofu (yureta), kibofu cha mkojo na njia ya mkojo inayotoka kwenye kibofu hadi nje ya mwili(yurethra). Maambukizi ya bakteria huweza kuathiri sehemu yoyote ya mfumo huu.
Mawe kwenye figo
Mawe kwenye figo hutengenezea na chumvichumvi zinazotokana na mkojo. Kuna dalili zingine nyingi zinaweza kuambtana na mawe kwenye figo kama vile maumivu makali upande mmoja wa figo yanayosambaa kuelekea kwenye mrija wa mkojo, pamoja na kutoa mkojo weusi. Kusoma dalili zingine zaidi ingia kwenye makala husika shemu nyingine katika tovuti hii
Kuvimba kwa tezi dume
Tezi dume inapatikana chini kidogo ya shingo ya kibofu cha mkojo cha mwanaume. Kazi yake kubwa nikutengeneza maji maji ya uzazi mwanaume(shawahawa). Wanaume wenye tezi iliyokuwa wengi wao hupata mkojo mchafu lakini hata hivyo mara nyingi huambatana na maambukizi.
Saratani ya kibofu
Seli hai za mwili huzaliwa na zilizozeeka au kuharibika kwa maradhi hufa kila siku, chembechembe zinazounda tezi dume pia hufa na nyingne huundwa kila siku kuchukua nafasi ya seli zilizokufa. Kama hakuna tatizo basi kitendo hiki hufanyika bila kuleta uvimbe na endapo kuna shida katika uuaji wa chembe zilizokufa au kuzaliswha kwa chembe za tezi ambazo hazina sifa na tabia kama chembe asili, chembe hizo huwa na sifa ya kuitwa saratani na husababisha kutokea kwa kwa uvimbe kwenye tezi dume.
Kupungukiwa maji mwilini
Ni pale mwili unapopoteza kiwango au kiasi kingi cha maji mwilini kwa njia mbalimbali ikiwepo jasho, kuharisha na mkojo mwili hupungukiwa maji na mtu huyu huambiwa kapungukiwa maji
Magonjwa ya zinaa
Ni magonjwa yanayo ambukizwa kwa njia ya kujamiana kama, mfano wake ni kisonono na kaswende. magonjwa mengi ya zinaa hupelekea kupata mkojo mchafu na wakati mwignine mkojo wenye usaha
Damu kwenye mkojo
Endapo kuna damu kwenye mkojo ambayo haionekani kwa macho ya kibinadamu, mkojo pia utaonekana kuwa mzito au kuwa na uchafu. Kukojoa damu inaweza kusababishwana maambukizi au magonjwa ya mfumo wa mkojo.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022 19:26:39
Rejea za mada hii
1. Medically reviewed by Judith Marcin, M.D – Written by Corinne O’keefe Osborn update on March 8, 2019.
2. Cloud urine:Symptoms and sings-Medica author ; Mellisa Conrad Stoppler, MD.Medically Reviewed on 9/10/2019
3. Top causes of cloud urine, from health concerns to your diet by Kathleen Smith, PhD, LPC,.Medically Reviewed by Dr. Robert Jasmer, MD,Last update; September 25,2018