Imeandikwa na ULY CLINIC
20 Septemba 2021, 12:33:53
Uono wa shimoni

Uono wa shimoni ni upotevu wa uwezo wa macho kuona vitu vya pembeni na kusalia na uwezo wa kuona vitu vya kati tu.
Kupoteza uwezo wa kuona vitu vya pembeni hufanya mgonjwa awe na uono mithiri ya mtu anayechungulia upande wa pili kupitia matundu madogo mawili ya duara au kuchungulia kitu kupitia bomba refu lenye kipenyo kidogo.
visababishi
Baadhi ya magonjwa yanayoweza kusababisha uono wa shimoni ni;
Glaukoma
Nyuropathi ya kisukari
Retinitis pigmentosa
Kuishiwa damu au maji
Matumizi ya pombe
Kutumia dawa kundi la Hallucinogen
Matumizi ya amphetamines
Hofu kuu au mshiko wa hofu
Furaha kuu inayofanya uzalishaji wa adrenaline
Homa ya kwenye mwinuko
Saratani ya pituitary zu zingine zinazogandamiza mshipa wa fahamu wa optic
Ugonjwa mkali wa mtoto wa jicho
Kuwa kwenye aura kwa mgonjwa wa kipanda uso
Hasira kali zinazofuatiwa na ongezeko kubwa la hormone adrenaline
Kung’atwa na nyoka mweusi (black mamba) au wengine wenye sumu kama yeye
Kudhuriwa na zebaki
Kunyimwa usingizi
Sindromu ya Usher
Kuzimia
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:21:19
Rejea za mada hii
Medical news today. What causes tunnel vision, and what are the treatments?. https://www.medicalnewstoday.com/articles/tunnel-vision#glaucoma. Imechukuliwa 20.09.2021
Eye institute. Tunnel Vision. https://www.eyeinstitute.co.nz/about-eyes/a-to-z-of-eyes/symptoms/tunnel-vision#. Imechukuliwa 20.09.2021
Iris Vision. https://irisvision.com/what-is-tunnel-vision-causes-symptoms-and-treatments-for-peripheral-vision-loss/. Imechukuliwa 20.09.2021
Cx Hu et al. Tunnel vision. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4206382/. Imechukuliwa 20.09.2021