top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

29 Machi 2020 11:43:36

Dalili za Kifaduro (Patusisi)
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za Kifaduro (Patusisi)

Kifaduro ikijulikana kitiba kama pertusis (patusisi) ni maambukizi katika mfumo wa juu wa hewa yanayosababishwa na bakteria anayeitwa Bordetella pertussis.


Maambukizi huambatana na uvimbe ndani ya Koo, hivyo huathiri upumuaji wa kawaida na kuleta dalili za kikohozi kikali kama cha kubweka, sauti za straida na kukauka kwa sauti.


Watu wakubwa dalili zinaweza kuwa za wastani, endapo mtu hakuwahi kupata chanjo dalili huwa ni kali, kwa watoto wadogo dalili huweza kuwa kali zaidi na kuleta madhara makubwa endapo asipopata matibabu.


Kifaduro ni ugonjwa mmojawapo ambao unatokea kwa mlipuko, lakini kutokana na ugunduzi wa chanjo yake, milipuko ya ugonjwa huu kwa sasa imepungua na watoto wachache huumwa kifaduro haswa wale ambao hawajapata chanjo au ambao chanjo imeisha nguvu.


Kifaduro huweza kuambatana na dalili za wastani , kiasi au Kali zinazozidi zaidi wakati wa usiku.

Ugonjwa huu huwapata Watoto wadogo ambao hawajapata chanjo au vijana wadogo ambao chanjo yao imeisha. Uchukua siku 10 kuanza kuonyesha dalili mara baad aya kupata maambukizi.


Vimelea vinavyosababisha kifaduro


  • Bordetella pertussis

  • Bordetella parapertussis


Vimelea wanaosababisha kifaduro huenezwaje?


  • Kwa njia ya hewa

  • Kwa njia ya kusogeleana (mawasiliano ya karibu na mtu aliye ambukizwa).

  • Kwa njia ya kugusa vimiminika vya mwili. mfano mate, mafua, na majimaji ya chafia.

  • Kwa njia ya kushika sehemu yenye virusi ambayo mtu amegusa mfani; mlango, nguo


Dalili za kifadulo


  • Homa

  • Kikohozi kikali

  • kutoa machozi na macho kuwa mekundu

  • Kuziba kwa pua

  • Kupata shida wakati wa kupumua/ kupumua haraka

  • Mwili kuchoka (uchovu)

  • Kuwashwa koo

  • Kupiga chafya


Madhara ya kifaduro


  • Nimonia

  • Henia

  • Kutokwa na damu puani

  • Otaitiz(Kuumwa kwa masikio)

  • Kuishiwa maji mwilini

  • Degedege

  • Kifo

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Pertussis frequently asked questions. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/pertussis/about/faqs.html. Imechukuliwa 25.03.2020

2.Kasper DL, et al., eds. Pertussis and other Bordatella infections. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 25.03.2020

3.Cornia P, et al. Pertussis infection in adolescents and adults: Clinical manifestations and diagnosis. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 25.03.2020

4.Yeh S. et al. Pertussis infection in infants and children: Clinical features and diagnosis. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 25.03.2020

5.Yeh S. Pertussis infection in infants and children: Treatment and prevention. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 25.03.2020

bottom of page