top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

29 Machi 2020 08:49:03

Dalili za kifo kukaribia
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za kifo kukaribia

Ni vigumu wakati mwingine kutabiri kwamba mtu atakufa lini. Hata hivyo mtu anayekaribia kufa huonyesha ishara zinazoashiria mwisho wa Maisha yake unakaribia.


Ishara za mtu anayekaribia kufa


Ishara zifuatazo zinaweza kuonekana kwa mpendwa na kumaanisha mwisho wa Maisha yake umekaribia;


  • Kuwa msumbufu na mkali

  • Kujitenga na watu

  • Kusinzia

  • Kukosa hamu ya kula na kunywa maji

  • Mabadiliko ya upumuaji na mapigo ya moyo

  • Kuona wafu

  • Kupata nguvu mpya


Kuwa msumbufu na mkali


Mtu anaweza kutotulia na kubadilisha pozi la kulala mara kwa mara au kutaka kushuka kwenye kitanda.


Kujitenga na watu


Kujitenga dhidi ya vitu anavyopenda kuvifanya na marafiki.


Kusinzia


Anaweza kuwa anasinzia sana au kulala usingizi na kushituka shituka mara kwa mara.


Kukosa hamu ya kula na kunywa maji


Huweza kula na kunywa kidogo kuliko kawaida


Mabadiliko ya upumuaji na mapigo ya moyo


Mapigo ya moyo hubadilika na hali ya upumuaji wa shida huonekana


Kuona wafu


Mpendwa hutoa taarifa kuwa ameona mtu aliyekufa zamani au kuongea nao, wakati mwingine mpendwa husema kuwa anakaribia kufa. Ishara hii kama inamfanya awe na furaha usibishane na mgonjwa kuepuka mizozo.


Kupata nguvu mpya


Mpendwa anaweza kupata nguvu mpya na za ghafla na wakati mwingine kuamka au kuwa kama mtu aliyepona kabisa. Hii inaweza kuwafikirisha watu kuwa matibabu yamefanya kazi au mgonjwa anaendelea vizuri. Hii si kweli bali ni moja ya kiashiria cha kufa. Kama hali hii ikitokea chukua fursa ya kuongea na mpendwa na kumwambia maneno ya mwisho.


Kumbuka


Ingawa ni vigumu kuzuia kifo kutokea, mpendwa huyu anahitaji kupewa ushirikiano na upendo wakati huu. Unatakiwa kushirikiana pamoja na wataalamu wa matibabu ya kupunguza maumivu au tiba nyumbani.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Bailey FA, et al. Palliative care: The last hours and days of life. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 28.09.2020

2.Institute for Clinical Systems Improvement. Palliative care for adults. Bloomington, Minn: Institute for Clinical Systems Improvement. https://www.guideline.gov/summaries/summary/47629/palliative-care-for-adults. Imechukuliwa 28.09.2020

3.Miller RD. Palliative medicine. In: Miller's Anesthesia. 8th ed. Philadelphia, Pa: Saunders Elsevier; 2015. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.09.2020
Kreher M. Symptom control at the end of life. Medical Clinics of North America. 2016;100:1111.

4.Providing comfort at the end of life. National Institute on Aging. https://www.nia.nih.gov/health/publication/end-life-helping-comfort-and-care/providing-comfort-end-life. Accessed Feb. 5, 2017.

bottom of page