Mwandishi:
Mhariri:
ULY Clinic
25 Juni 2020 18:07:12
Dalili za kiharusi
Stroku hutokana na kufa kwa seli za ubongo kwa sababu ya kukosa oksijeni ya kutosha pale ambapo damu haifiki kwenye ubongo kwa sababu sababu mbalimbali. Sababu huenda ikawa ni kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu inayoenda kwenye ubongo.
Visababishi
Kuvilia kwa damu ndani ya ubongo
Kutofika kwa damu kwenye ubongo kwa kiwango kinachotakiwa
Vihatarishi vya kupata kiharusi
Wembamba wa mishipa inayopitisha damu kwenye ubongo
Shinikizo la juu la damu
Ugonjwa wa kisukari
Maambukizi kwenye mishipa ya damu
Uvutaji wa sigara
Uwepo wa histroria ya ugonjwa wa stroke kwenye familia
Umri mkubwa
Matumizi mabovu na ya mda mrefu ya pombe
Uwepo wa kolestro kwenye mishipa ya damu
Matatizo ya moyo{moyo kufeli}
Kukakamaa kwa Mishipa ya damu ya kwenye ubongo.
Dalili za kiharusi
Kushindwa kusoma
Kushindwa kuandika
Kushindwa kumeza
Kushindwa kutembea
Kukosa balansi ya mwili
Kichefuchefu na Kutapika
Kupooza Mwili
Degedege
Kuumwa na kichwa
Kushindwa kuhisi na ganzi.
Kupoteza fahamu
Namna ya kujikinga na kiharusi
Unaweza kujikinga na kiharusi kwa
Kuboresha mtindo wa maisha, ishi kama unavyoshauriwa na mtaalamu wa afya kwa kula chakula bora chenye afya pamoja na kufanya mazoezi yenye mpangilio maalumu
Kuepukana na matumizi pombe na sigara
Kupima presha mara kwa mara
Kwa wagonjwa wa presha inatakiwa watumie dawa vizuri.
Kuzingatia kanuni za Afya zinazotolewa na wataalamu wa Afya.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021 04:52:15
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Braunwald, E. & Fauci, A.S. (2001). Harrison’s Principles of Internal Medicine. McGraw Hill.
2.Cumming, A.D. (2008). Davidson’s Principles and Practice of Medicine. Churchill Livingstong.
3.Goldstein, L.B. (2007). Braunwald's Heart Disease. Edinburgh: Oxford.
4.Kumar, P. & Clark, M. (2007). Clinical Medicine. Edinburgh: Elsevier Saunders
5.Zivin, J.A. (2007). Hemorrhagic Cerebrovascular Disease. Cecil Medicine. Philadelphia: Saunders Elsevier.