top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

7 Julai 2021, 18:54:21

Hedhi yenye damu kidogo
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Hedhi yenye damu kidogo

Kwa kawaida, mwanamke hupoteza kiasi cha mililita 5 hadi 80 za damu kwenye kila hedhi. Kupoteza kiasi chini ya mililita 30 za damu hufahamika kama ‘hedhi yenye damu kidogo' au 'haipomenorea' au. Kuna visababishi vya aina kadhaa vya hedhi yenye damu kidogo kama vilivyoorodheshwa hapa chini.


Visababishi


Visababishi vya hedhi yenye damu kidogo mara nyingi huhusiana na mambo ya homon pamoja na madhaifu ya via vya uzazi ambayo vinaweza kuwa;


  • Ujauzito

  • Ufanyaji kazi m'bovu wa tezi thyroid

  • Matumizi ya homon za uzazi wa mpango

  • Ongezeko kubwa la uzito

  • Msongo wa mwilin

  • Makovu ndani ya uzazi

  • Sindromu ya ovari yenye vifuko maji vingi

  • Kuingia koma hedhi

  • Kusinyaa kwa shingo ya kizazi

  • Kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua


Maelezo kwa kina yanapatikana kwenye aya zinazofuata


Ujauzito

Ujauzito kwa kawaida husababisha kutoona damu ya hedhi, hata hivyo huweza ambatana na damu kidogo ya hedhi kwa baadhi ya wanawake, hedhi hii huwa nyepesi na yenye damu kidogo. Baadhi ya nyakati kutokwa na hedhi yenye damu kidogo au matone ya dam utu huweza kuwa dalili ya ujauzito nje ya kizazi( mimba ya ekitopiki) ambao ni hatari na unahitaji matibabu ya dharura.


Umeongezeka uzito kupita kiasi

Mabadiliko ya uzito huambatana na mabadiliko ya hedhi, hii ni kwa sababu kuongezeka uzito inamaanisha kuongezeka mafuta mara nyingi. Mafuta haya ni chanzo kizuri cha kutengeneza homoni mwilini.


Msongo mwilini

Msongo mwilini huweza kusababisha magonjwa mengi, ikiwa pamoja na mabadiliko ya homon mwilini. Unaweza kuwa na mambo mengi yanayokusonga au ambayo hayana majibu hivyo kukusababisha ongezeko la homon za msongo ambazo huingiliana na homon za kike zinazorekebisha mzunguko wa hedhi. Mfano wa visababishi vya msongo ni, kuombolezwa kwa aliyeachwa au kufiwa, kufanya mazoezi makali n.k


Ufanyaji kazi m'bovu wa tezi thyroid

Ufanyaji kazi kupitiliza wa tezi thyroid, tezi ndogo mbele ya shingo yako, husababisha uzalishaji wa homon thyroid za kwa wingi ambazo huwa na madhara kwenye moyo, shinikizo la damu, misuli n.k. mwathirika anaweza kuwa na dalili zingine mbali na kutoona hedhi au kuwa na damu kidogo ya hedhi. Soma zaidi kwenye Makala ya hapathairoidizimu.


Matumizi ya homon za uzazi wa mpango

Kisababishi kikuu cha watu wengi wanaotumia dawa za uzazi wa mpango huwa ni kukosa hedhi au hedhi yenye damu kidogo. Baadhi ya wataalamu madhara ya vidonge hivi kwa matibabu ya hedhi yenye damu nyingi. Endapo una hedhi kidogo na unatumia njia za uzazi wa mpango zenye homon kama dawa, vipandikizi, njiti au kuchoma sindano ya depoprovera n.k, hiyo inaweza kuwa kisababishi.


Sindromu ya ovari yenye vifuko maji vingi

Sindromu hii huambatana na uzalishaji wa homon za kiume nyingi zaidi zenye jina la androjen kama vile testosterone. Homon za kiume husababisha mwili wa mwanamke kuwa na nywele nyingi(ndevu), misuli, kuongezeka uzito, kuota chunusi na kupunguza au kuzuia damu ya hedhi na wakati mwingine kuzuia kutengenezwa kwa mayai. Kuwa na sindromu hii pia huweza kupelekea hedhi kuwa kubwa.


Kuingia kipindi cha koma hedhi

Dalili moja wapo ya kuingia koma hedhi ni kuwa na hedhi ambazo zinachukua muda mrefu kutokea au kuwa na damu kidogo, hata hivyo wakati mwingine unaweza kuwa na vipindi vya damu nyingi ya hedhi. Endapo unakaribia oma hedhi unaweza kuwa na dalili ya kuona hedhi yenye damu kidogo.


Kusinyaa kwa shingo ya kizazi

Hii hutokea kwa nadra sana kwa wanawake, shingo ya kizazi inaposinyaa husababisha njia ya kutoa damu kuwa kidogo au kuziba kabisa na hivyo damu ya mwezi kutoka kwa shida au kutotoka kabisa. Kisababishi cha kusinyaa kinaweza kuwa kufanyiwa upasuaji wa shingo ya kizazi kama ule wa kuimarisha shingo ya kizazi ili mimba isitoke au kukatwa nyama kwa ajili ya kipimo cha pap smia, au kukwanguliwa kizazi kama tiba ya hedhi nzito au kwa sababu ya matatizo ya homon wakati wa kuingia koma hedhi.


Makovu ndani ya uzazi

Endapo umefanyiwa upasuaji mwingi wa kukwangua kizazi kwa ajili ya kutoa mimba, hii inaweza leta makovu ndani ya kizazi na matokeo yake ni kuwa na damu kidogo ya hedhi. Makovu mengi sana kwenye kizazi huweza pelekea kupata sindromu ya asherman’s ambao huwa na dalili ya kukosa hedhi au hedhi yenye damu kidogo sana.


Kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua

Kupoteza damu nyingi sana wakati wa kujifungua husababisha sindromu ya sheehans. Sindromu hii hutokana na kuharibika kwa tezi pituitari kwa sababu ya kukosa kiasi cha kutosha cha damu na hivyo hushindwa kuzalisha homon vema ambazo zinashughulika na matendo mengi ikiwa pamoja na mzunguko wa hedhi.


Dalili


Dalili kuu ya damu kidogo ya hedhi ni kutokwa na matone kidogo ya damu wakati wa hedhi


Wakati gani wa kuonana na daktari?


Unapokuwa na hedhi kidogo au damu kidogo wakati wa hedhi, huna haja ya kuogopa kwa mara ya kwanza, unachotakiwa kufanya ni kuchunguza hedhi yako kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu. Endapo shida inaendelea, wasiliana na daktari kwa uchunguzi na tiba. Onana na daktari haraka endapo;


  • Hedhi yako imekuwa haieleweki kwa ghafla

  • Hujapata hedhi miezi mitatu mfululizo

  • Unapata mzunguko wa hedhi wa chini ya siku 21 au kwa zaidi ya siku 35

  • Unapata hedhi yenye maumivu makali sana

  • Unapata hedhi inayodumu zaidi ya wiki

  • Unafikiria kuwa una ujauzito


Vihatarishi


Vihatarishi vifuatavyo uwezekano wa kupata hedhi yenye damu kidogo;


  • Uwepo wa tatizo hili kwenye familia- hii inawezekana ikamaanisha ni tatizo la kurithi

  • Matumizi ya muda mrefu ya uzazi wa mpango wenye homon

  • Umri mkubwa

  • Kufanya mazoezi makali

  • Kuugua kisukali

  • Matumizi ya pombe yaliyokithiri na uvutaji wa sigara

  • Ugonjwa wa obeziti

  • Kula mlo duni usio na makundi yote ya chakula


Uchunguzi


Mara baada ya kuonana na daktari wako, utaulizwa maswali ya kitiba yakiwa na lengo la kutambua dalili zingine, kisababishi na vihatarishi mbalimbali ulivyonavyo. Baada ya hapo daktari ataagiza ufanye vipimo kulingana na nini alichoona kuwa kisababishi. Vipimo hivyo vinaweza kuwa;


  • Kipimo cha picha halisi ya homon mwilini

  • Kipimo cha picha sauti ya via vya uzazi

  • Kipimo cha kamera ya kuangalia ndani ya via vya uzazi

  • Kipimo cha CT scan au MRI ya mfumo wa uzazi au tezi ya thyroid na pituitary


Matibabu


Matibabu ya hedhi yenye damu kidogo hulenga kisababishi kama vilivyoorodheshwa kwenye Makala hii. Matibabu huweza kuhusisha matumizi ya dawa au upasuaji. Unaweza kusoma kwenye Makala moja moja ya kila kisababishi ili kufahamu ni namna gani matibabu yanafanyika.


Tiba asilia ya hedhi yenye damu kidogo

Kuna baadhi ya dawa asilia zenye uwezo wa kurekebisha matatizo ya homon ambayo hupelekea kupata hedhi yenye damu kidogo. Hata hivyo unahitaji kufanyiwa uchunguzi kwanza na daktari wako ili kufahamu shida ni nini kabla ya kutumia dawa hizo.


Matibabu ya nyumbani

Mambo yafuatayo yana ushahidi wa kisayansi kusadia wanawake wenye hedhi yenye damu kidogo au hedhi kidogo katika mwaka.


  • Kufanya mazoezi ya yoga

  • Kuwa na uzito wa kiafya( uzito kulingana na BMI)

  • Kufanya mazoezi ya mpangilio

  • Kula vyakula vyenye tangawizi au mdalasini

  • Kutumia dozi ndogo ya vitamin D na B

  • Kunywa juisi ya tufaa iliyochachushwa ( vinegar ya tufa) unayoweza kuchanganya na nanasi

  • Kula nanasi


Majina mengine ya damu kidogo ya hedhi

Hedhi yenye damu kidogo hufahamika kwa majina mengine ya;


  • Hedhi kidogo

  • Mizunguko michache ya hedhi

  • Kutokwa na damu kidogo wakati wa hedhi

  • Hedhi ndogo

  • Hedhi yenye damu kidogo

  • Hedhi isiyo na damu

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021, 05:23:12

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Mariam Mathew, et al. Recurrent Cervical Stenosis – a Troublesome Clinical Entity. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3282328/. Imechukuliwa 07.07.2021

2. Aparecida Cristina Sampaio Monteiro, et al. Cervical stenosis following electrosurgical conization. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/18853028/. Imechukuliwa 07.07.2021

3. Klein DA, et al. Amenorrhea: A systematic approach to diagnosis and management. American Family Physician. 2019; https://www.aafp.org/afp/2019/0701/p39.html. Imechukuliwa 07.07.2021

4. Goldman L, et al., eds. Reproductive endocrinology and infertility. In: Goldman-Cecil Medicine. 26th ed. Elsevier; 2020. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 07.07.2021

5. Kellerman RD, et al. Amenorrhea. In: Conn's Current Therapy 2021. Elsevier; 2021. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 07.07.2021

6. Gordon CM, et al. Functional hypothalamic amenorrhea: An Endocrine Society clinical practice guideline. Journal of Clinical Endocrinology and Metabolism. 2017; doi:10.1210/jc.2017-00131.

7. Hypomenorrhea Treatment in Indian Women: An In-depth Explanation. https://www.mfine.co/guides/hypomenorrhea-treatment-indian-women/. Imechukuliwa 07.07.2021

8. JoAnn V. Pinkerton MD.. Overview of Menstrual Disorders. https://www.msdmanuals.com/home/women-s-health-issues/menstrual-disorders-and-abnormal-vaginal-bleeding/overview-of-menstrual-disorders. Imechukuliwa 07.07.2021

9. Collin Smikle, et al. Asherman Syndrome. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK448088/. Imechukuliwa 07.07.2021

10. Mark P. Schury, et al. Sheehan Syndrome. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK459166/. Imechukuliwa 07.07.2021

11. Uche Anadu Ndefo, et al. Polycystic Ovary Syndrome. A Review of Treatment Options With a Focus on Pharmacological Approaches. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3737989/. Imechukuliwa 07.07.2021

12. Simone De Leo, et al. Hyperthyroidism. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5014602/. Imechukuliwa 07.07.2021

13. Nanette Santoro, MD, et al. Perimenopause: From Research to Practice. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4834516/. Imechukuliwa 07.07.2021

14. Hypermenorrhea. https://europepmc.org/article/med/12561709. Imechukuliwa 07.07.2021

15. Vungarala Satyanand, et al. Effects of Yogasanas in the Management of Pain during Menstruation. https://www.researchgate.net/publication/268983506_Effects_of_Yogasanas_in_the_Management_of_Pain_during_Menstruation. Imechukuliwa 07.07.2021

16. Christina E. McGovern RN, BSN, PHN, et al. Yoga and Quality of Life in Women with Primary Dysmenorrhea: A Systematic Review. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/abs/10.1111/jmwh.12729. Imechukuliwa 07.07.2021

17. Kyung Min Ko, et al. Association between Body Weight Changes and Menstrual Irregularity: The Korea National Health and Nutrition Examination Survey 2010 to 2012. https://www.e-enm.org/journal/view.php?doi=10.3803/EnM.2017.32.2.248. Imechukuliwa 07.07.2021

18. Shuying Wei, et al. Obesity and Menstrual Irregularity: Associations With SHBG, Testosterone, and Insulin. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/full/10.1038/oby.2008.641. Imechukuliwa 07.07.2021

19. Zahra Mohebbi Dehnavi, et al. The Effect of aerobic exercise on primary dysmenorrhea: A clinical trial study. https://www.jehp.net/article.asp?issn=2277-9531;year=2018;volume=7;issue=1;spage=3;epage=3;aulast=Dehnavi.Imechukuliwa 07.07.2021

20. Farzaneh Kashefi, et al. Effect of Ginger (Zingiber officinale) on Heavy Menstrual Bleeding: A Placebo-Controlled, Randomized Clinical Trial. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/abs/10.1002/ptr.5235. Imechukuliwa 07.07.2021

21. Samira Khayat, et al. Effect of Treatment with Ginger on the Severity of Premenstrual Syndrome Symptoms. https://academic.oup.com/painmedicine/article/16/12/2243/2460294. Imechukuliwa 07.07.2021

22. James W. Daily, Ph.D, et al. Efficacy of Ginger for Alleviating the Symptoms of Primary Dysmenorrhea: A Systematic Review and Meta-analysis of Randomized Clinical Trials. https://www.hindawi.com/journals/isrn/2014/792708/. Imechukuliwa 07.07.2021

23. Kassandra L Munger, et al. Serum 25-hydroxyvitamin D levels and risk of multiple sclerosis. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/17179460/. Imechukuliwa 07.07.2021

24. Anne Marie Z Jukic, et al. Lower plasma 25-hydroxyvitamin D is associated with irregular menstrual cycles in a cross-sectional study. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/25879830/. Imechukuliwa 07.07.2021

25. Farideh Shishehbor, et al. Vinegar consumption can attenuate postprandial glucose and insulin responses; a systematic review and meta-analysis of clinical trials. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/28292654/. Imechukuliwa 07.07.2021

bottom of page