Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
28 Desemba 2020 14:25:05
Kupungua uzito bila sababu
Kupungua uzito bila sababu ni hali inayoweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali, yakiwa ni magonjwa ya kisaikolojia au maambukizi au saratani ndani ya mwili. Mara nyingi kupungua uzito bila sababu hutokea katika kipindi kirefu haswa zadi ya wiki au miezi kadhaa, hali hii huweza ongeza hatari ya kupata madhara makubwa au kifo.
Makala hii imejikita kuzungumzia maana, dalili, visababishi vipimo na matibabu ya tatizo la kupungua uzito bila sababu.
Makala ya kupungua uzito kwa kujitakia imezungumziwa shemu nyingine katika tovuti hii ya ULY CLINIC.
Maana
Mtu atasemekana kuwa amepungua uzito bila sababu endapo endapo amepungua Zaidi ya asilimia 5 ya uzito wake au kupungua kilo 5 ndani ya kipinid cha miezi sita. Maana hii inaweza isiwe sahihi kwa watu walio na ugonjwa wa moyo kuferi kufanya kazi n.k
Tatizo la kupungua uzito bila sababu hutokea haswa pale endapo mtu anakosa hamu ya kula na wakati huo mwili wake unatumia nguvu nyingi kutoka kwenye virutubisho vilivyo ndani ya mwili mfano kutoka kwenye mafuta na misuli.
Dalili
Baadhi ya wagonjwa wenye dalili hii wanaweza kuwa na dalili hii zingine zinazoambatana ambazo ni;
Anorexia
Homa
Kutokwa na jasho wakati wa usiku
Dalili za uunguu wa virutubisho muhimu mwilini
Visababishi
Visababishi vimegawanyika katika makundi mengi, makala hii imezungumzia makundi mawili ambavyo ni
Visababishi vinavyoonekana wazi kama magonjwa yanayosababisha kuhara kwa muda mrefu au visababishi visivyo vya wazi kama vile saratani isiyofahamika ndani ya mwili n.k.
Visababishi vinavyoongeza hamu ya kula
Visababishi vinavyoongeza hamu ya kula lakini unapungua uzito ni;
Ugonjwa wa Kisukari usiodhibitiwa
Ugonjwa wa Hyperthyroidism
Magonjwa yanayosababisha kutofyonzwa kwa chakula tumboni
Visababishi vinavyopunguz ahamu ya kula
Visababishi vinavypunguza hamu ya kula lakini unapungua uzito ambavyo ni;
Magonjwa ya akili kama msongo wa mawazo au sonona
Saratani aina yoyote
Madhara ya maudhi ya dawa
Kutumia dawa za kulevya
Visababishi vingine
Visababishi vingine kwa ujumla ni pamoja na;
Upasuaji wa tumbo na utumbo
Ugonjwa wa cystic fibrosis
Magonjwa sugu ya inflammation tumboni
Baridi yabisi
Ugonjwa wa Achalasia,
Ugonjwa wa celiac na Crohn
Ugonjwa sugu wa pancreatitis
Magonjwa ya mrija wa esophagus
Ugonjwa wa ischemic colitis
Ugonjwa wa diabetic enteropathy
Ugonjwa wa vidonda vya tumbo
Ugonjwa wa ulcerative colitis katika hatua za mwisho
Magonjwa sugu ya moyo na mapafu kama vile kuferi kwa moyo, COPD
Magonjwa ya akili kama vile Anxiety, bipolar disorder, depression, schizophrenia
Magonjwa ya mfumo wa fahamu kama vile Amyotrophic lateral sclerosis, dementia, multiple sclerosis,
myasthenia gravis, Parkinson disease, stroke
Matatizo ya kijamii kama vile umasikini na kutengwa
Wakati gani utafute msaadawa kiafya wa dharura?
Dalili za kufanya utafute msaada wa haraka ni;
Homa
Kutokwa na jasho nyakati za usiku
Kuvmba kwa mitoki
Maumivu ya mifupa
Kushindw akupumua
Kukohoa damu
Kutapika damu
Kuogopa kuongezeka uzito kwa mabindi au vijana wadogo
Kukojoa sana na kunywa maji sana
Maumivu ya kichwa, kupotea kwa uono kwa watu wazima
Kupata Madoa ya Roth spot, Janeway lesions, Osler nodes na kuvilia kwa damu chini ya kucha splinter hemorrhages
Vipimo
Endapo una tatizo la kupungua uzito bila sababu, utakapofika hospitali utaulizwa maswali mengi yanayolenga kufahamu tatizo lako na kisha daktari wako ataagiza ufanye vipimo vya msingi ili kutambua ni nini kisababishi kwako. Utafanyiwa vipimo pia vya kutambua saratani mbalimbali zinazoshukiwa kama kipimo cha kamera kutazama ndnai ya utumbo- colonoscopy au kipimo cha mammography. Vipimo vingine vya awali ni;
Complete blood count (CBC) na differential count
Erythrocyte sedimentation rate (ESR) au C-reactive protein
HIV
Kiwango cha thyroid-stimulating hormone (TSH)
Serum chemistries (serum electrolytes, calcium, hepatic na renal function tests)
Urinalysis
x-ray ya kifua
Matibabu
Matibabu ya kupungua uzito bila sababu hutegemea kisababishi ambacho kitafahamika
Matibabu ya nyumbani
Matibau ya nyumbani yanahusisha;
Kama shida ni kula mlo kamili, mgonjwa anashauriwa kutumia chakula chenye mlo kamili kama kilivyoelezewa sehemu nyingine katika tovuti hii. Fanya hivi kwa kumsititiza na kumlisha mgonjwa, mpatie vyakula vyenye nyama, wanga, matunda na mboga za majani na milo mingi ya katikati kabla yam lo mkuu na kabla ya kulala usiku. Mpatie mgonjwa chakula anachokipendelea Zaidi na kwa kiasi kidogo kidogo.
Endapo mgonjwa anashindwa kumeza chakula au kuna kizuizi cha chakula kuingia tumboni, mgonjwa anapaswa kuwekewa mpira kwa ajili ya kumlisha vema.
Pima uzito wa mwili kila siku ili kuangalia mabadiliko katika uzito wa mgonjwa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.MSD manual. Involuntary Weight Loss. https://www.msdmanuals.com/professional/special-subjects/nonspecific-symptoms/involuntary-weight-loss. Imechukuliwa 28.11.2020
2.Evans AT, et al. Approach to the patient with unintentional weight loss. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.11.2020
3.Ferri FF. Weight loss, unintentional. In: Ferri's Clinical Advisor 2018. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.11.2020
4.Ritchie C, et al. Geriatric nutrition: Nutritional issues in older adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.11.2020