top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Sslome A, Md. Dkt. Sospeter B, MD

9 Februari 2024 15:12:36

Macho mekundu
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Macho mekundu

Ugonjwa wa jicho au macho mekundu ni tatizo linalojitokeza sana, huweza kuathiri jicho moja au macho yote na huweza kutokea katika mlipuko pia kulingana na ksiababishi. Hali hii hutokea pindi mishipa midogomidogo ya damu inapovimba au kupasuka kutokana na mambukizi au uchokozi (umwingiliano) katika jicho katika jicho.


Vyanzo vya kawaida vya jicho jekundu ni maambukizi na mzio na wakati mwingine huashiria tatizo kubwa la macho kama jeraha kwenye jicho, presha ya juu kwenye macho (glaukoma) n.k.


Hali ya macho mekundu huweza kuisha bila kuacha athari yoyote katika macho kwa matibabu ya nyumbani, hata hivyo ikiwa hali hii imeambatana na dalili kama kupungua kwa uono, maumivu makali, kuogopa mwanga nk unapaswa kupata msaada wa kitabibu.


Visababishi vya macho mekundu

Zifuatazo ni sababu za macho mekundu zinazojitokeza sana:

  • Maambukizi (hasa konjaktivaitisi na trakoma)

  • Mzio wa macho

  • Ukavu wa macho

  • Jeraha kwenye jicho

  • Kidonda kwenye Konea

  • Ugonjwa wa glaukoma

  • Sindromu ya kutumia kopmyuta


Dalili na viashiria vya macho mekundu

Dalili kuu ni rangi ya sehemu ya mbele ya jicho(konea) nyeupe ya jicho kuwa nyekundu, pia inaweza kuambatana na dalili pamoja na viashiria vifuatavyo kulingana na kisababishi;

  • Muwasho

  • Kutoa machozi

  • Macho kuuma

  • Kutoa tongotongo

  • Mabadilio ya kuona kama vile kuona ukungu

  • Kuvimba kwa macho

  • Mafua na kupiga chafya

  • Kikohozi

  • Kuvimba kwa tezi za tonsesi


Matibabu ya nyumbani

Ikiwa una macho mekundu na dalili za kawaida kama muwasho, maumivu kwa mbali, mafua, na kupiga chafya unaweza kujitibia nyumbani kwa kufanya yafuatayo;

  • Loweka kitambaa kizito katika maji ya baridi juu ya macho yaliyofungwa, husaidia kupunguza uvimbe na wekundu

  • Safisha macho yako kwa maji safi

  • Unaweza kutumia dawa za kawaida kupunguza dalili, mfano dawa za maumivu kama panadol, na za machozi bandia

  • Punguza matumizi ya vifaa vya kieletroniki kama vile kishikwambi na kompyuta

  • Punguza au acha matumizi ya vipodozi mpaka utakapopona

  • Ikiwa kisababishi ni mzio, fanya uchunguzi kubaini viamsha mzio na uviepuke


Ni wakati gani wa kumuona daktari?

Unatakiwa kumuona daktari endapo macho mekundu yameambatana na dalili hizi;

Unapata maumivu makali ya macho

  • Viepele usoni hasa eneo linalozunguka jicho

  • Umeanza kuwa na uono hafifu au kuona ukungu

  • Kutokwa na tongotongo zinazoganda kwenye kope

  • Macho mekundu baada ya upasuaji wa macho

  • Macho mekundu kwa mtu anayevaa lenzi bandia

  • Macho kuvimba

  • Una dalili zaidi ya wiki na zimekuwa zikiendelea kuwa mbaya

  • Macho mekundu yameanza baada ya kuumia jicho

  • Unapata maumivu ya kichwa na kutapika, na kuona ukungu


Jinsi ya kujikinga na macho mekundu

Unaweza kupunguza hatari ya kupata macho mekundu kwa kufanya yafuatayo:

  • Epuka kugusa au kufikicha macho yako na mikono michafu

  • Usitumie lenzi bandia zaidi ya muda ulioshauriwa

  • Safisha lenzi kama inavyopendekezwa

  • Ondoa lenzi wakati wa kulala

  • Ondoa vizuri urembo (make up) katika macho yako na hakikisha ni masafi

  • Usitumie vifaa kama simu au kompyuta kwa muda mrefu bila kupumzisha macho yako

  • Jitahidi kuepuka vitu vinavyoweza kusababisha macho kuwa na umwingiliano mfano moshi, vumbi nk


Mambo ya kuzingatia

  • Macho mekundu huweza kuashiria ugonjwa flani wa macho au kama dalili ya ugonjwa usiohusiana moja kwa moja na macho.

  • Macho mekundu yanaweza kupona kwa matibabu ya nyumbani, fika hospitali ikiwa una dalili za hatari kama maumivu na mabadiliko ya uono.

  • Usijaribu kutumia dawa za macho bila ushauri wa daktari.

  • Unaweza kuepuka macho mekundu kwa kuzingatia kanuni za usafi hasa eneo la uso.


Majina mengine


Majina mengine ya makala hii ni

  • Macho kuwa mekundu

  • Ugonjwa wa macho mekundu

  • Ugonjwa wa jicho jekundu

  • Dalili ya jicho jekundu


Tahadhari

Usitumie dawa yoyote kujitibu mwenyewe bila ushauri wa daktari ili kuepuka madhara yanayoweza kusababisha kupoteza uono wa jicho.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

9 Februari 2024 15:15:02

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.     The red eye – first aid at the primary level - PMC – NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1705661/. Imechukuliwa 09.02.2024

2.      The red eye – PMC. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3017259/. Imechukuliwa 09.02.2024

3.      Red Eye - Eye Disorders - MSD Manual Professional Edition. https://www.msdmanuals.com/professional/eye-disorders/symptoms-of-ophthalmic-disorders/red-eye. Imechukuliwa 09.02.2024

4.      Red Eyes: 20 Causes, Symptoms, Complications, and More. Healthline. https://www.healthline.com/health/eye-redness. Imechukuliwa 09.02.2024

bottom of page