Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, MD
17 Novemba 2020, 19:52:30


Maumivu ya kifua yanayoanzia shingoni
Maumivu ya kifua yanayotokana na madhaifu ya shingo ni tatizo linalotoke na mara nyingi huchanganywa na wataalamu wa afya kuwa ni maumivu ya anjaina. Asilimia 50 ya wagonjwa wanaosemekana kuwa wana anjaina ya moyo huwa na spondilosisi ya seviko. Wagonjwa wengi wa aina hii hufanyiwa vipimo vya moyo visivyo vya lazima.
Makala hii imejikita kuangalia maumivu ya kifua kutokana na madhaifu ya shingo.
Madhaifu ya shingo yanayoweza kuleta maumivu ya kifua
Madhaifu ya shingo yanayoweza kuleta maumivu ya kifua ni;
Spondailosis ya sevaiko- katileji na mifupa ya shingo kuisha kusiko kawaida
Henia ya diski ya sevaiko- Kupasuka kwa diski kati ya mifupa ya shingo, kuchomoza kwa diski au kutoka kabisa kwa diski sehemu yake ya kawaida
Kukakamaa kwa ligament- Hutokanana kuzeeka kwa ligament, tatizo hutokea kwa jinsi mtu anavyokuwa na umri mkubwa zaidi
Stenosisi ya tundu la uti wa mgongo- Kupungua kwa kipenyo cha tundu la uti wa mgongo
Sevaiko mayelopathi- kuharibiwa kwa uti wa mgongo kutkana na kupungua kwa kipenyo au magonjwa ya kuzeeka kwa mifupa ya uti wa mgongo
Sevaiko nyuropathi/radikulopathi- kufinywa au kugandamizwa kwa mshipa wa fahamu
Stenosisi ya tundu la uti wa mgongo
Ni kupungua kwa kipenyo cha tundu la uti wa mgongo kutokana na magonjwa mbalimbali au kuzeeka kwa mifupa ya uti wa mgongo ya shingoni. Kukaa pozi baya na magonjwa ya maungio ya mifupa ya shingo kama athraitis huweza kusababisha tatizo hili. Visababishi vingine vinaweza kuwa kuumizwa kwa mifupa ya shingo kutokana na ajali, kupasuka kwa mishipa ya damu ya shingo, majeraha kwenye ligament, na maoteo ya mifupa kwenye mifupa ya shingo.
Dalili
Maumivu ya shingo au mkono
Ganzi au udhaifu wa mikono na viganja vya mkono
Kukazakwa misuli ya miguu
Kukosa mpaangilio mzuri wa mijongeo ya misuli kwenye mkono, kinganja cha mkono na vidole
Kutepweta kwa maungio ya mikono
Kulegea kwa misuli ya mokono/viganja vya mikono
Sevaiko radikulopathi
Ugonjwa huu unafahamika kwa jinga jingine kama sevaiko nyuropathi, hutokana na kubanwa kwa mishipa ya fahamu ya shingo. Kubanwa huku hutokana na kuzeeka, kuisha au majeraha katika maeneo ya shingo
Matibabu
Utapewa matibabu ya dawa au upasuaji kutokana na kisababishi cha tatizo lako. Wasiliana na daktari wako kwa vipimo na matibabu ya tatizo lako
Matibabu ya nyumbani
Matibabu ya nyumbani yanahusisha, kupunguza kazi ambazo zinapelekea dalili kuonekana zaidi, kuvaa kifaamaalumu cha kuzuia kuumia kwa shingo unapokuwa umekaa au unasafiri, kupumzika kwa muda, kufanyiwa masaji ya shingo, kukandwa kwa madhi ya moto au baridi na kutumia dawa za maumivu kama utakavyoshauriwa na daktari wako.
Kaa pozi zuri la kiafya acha kupindisha shingo na hakikisha miguu yote imegusa aridhi unapokuwa umekaa
Jifunze namna sahihi ya kunyanyua vitu vizito,usitumie mgongo kunyanyua vitu, chuchumaa unapotaka kuchukua na kunyanyua kitu badala ya kupindisha mgongo
Pumzika mara kwa mara unapokuwa unafanya kazi ya muda mrefu
Fanya mazoezi ya Uti wa mgongo, soma katika Makala zetu kwa maelezo zaidi kuhusu maumivu ya shingo.
Sevaiko spondailosis
Spondailosis ya sevaiko- hutokana kuisha kusiko kawaida kwa katileji inayozuia msuguano kati ya mfupa mmoja na mwingine katika shingo. Kuisha huku huweza kusababishwa na kuzeeka au magonjwa Fulani.
Dalili
Ugonjwa huu hutokea kwa watu wenye umri mkubwa zaidi na dalili zake huwa;
Maumivu ya shingo yanayoweza kusafirikwenye kwenye mabega na mkono
Maumivu ya kichwa
Kuhisi kusagika kwa mifupa ya shingo unapogeuza shingo
Kulegea kwa mikono na miguu
Ganzi kwenye maeneo ya mabega, mkono na kiganja cha mkono
Kukakamaa kwa shingo
Kushindwa kusiamama wima
Kushindwa kuzuia mkojo
Maumivu ya kifua
Mfano wa mgonjwa wa Sevaiko spondailosis
Tuangalie mgonjwa ambaye amewahi kuwa na maumivu ya kifua kutokana na sevaiko spondailosis
Mwanamke wa umwi wa miaka 53 alikuja hospitali akiwa na maumivu ya kifua na mgongo katikati ya mifupa ya mgongo na bega moja la kushoto. Maumivu yalikuwa yakuja na kuondoka au kubana na kila yalipotokea yalidumu kwa muda wa masaa mawili hadi matatu. Maumivu hayo yaliambatana na hisia za ganzi mkono wa kushoto hata hivyo hakuwa na dalili zozote zile za kubadilika kwa mfumo wa moyo kamavile mapigo ya moyo kwenda kasi, kushindwa kulala chali wakati wa usiku, kuishiwa pumzi kirahisi, kichefuchefu na kutapika. Mgonjwa alisema hanahistoria ya homa, kikohozi, miruzi kwenye kifua, kiungulia au kucheua. Miaka 20 iliyopita alipata maaambukizi ya herpes kifuani upande wa kushoto. Alishawahi kufanyiwa upasuaji wa kuondoa apendeksi na hana historia ya presha, kisukari, magonjwa ya moyo au mishipa ya damu na wala familia yake hakunamtu wmenye shida hii au hizi zilizotajwa.
Uchunguzi wa awali wa mwili ulionyesha hakuna shida yoyote mwilini
Vipimo vya moyo na kifua vilionyeshahakuna shida yoyote kwenye kifua
Mgonjwa alifanyiwa vipimo vingine vingi ikiwa pamoja na picha ya tumbo n.k lakini hakukuwa na shida.
Mwisho wa siku alifanyiwa kipimo cha MRI ya uti wa mgongo ameneo ya shigo, shida iliyoonekana ilikuwa ni sevaiko spondailosis na kuchomoza kwa diski katika mifupa ya shingo iliyopelekea kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu ya shingo na kusinyaa kwa tundu la uti wa mgongo kwa kiasi kidogo.
Mgonjwa alipatiwa dawa za maumivu jamii ya Cox 2 inhibita, dawa jamii ya PPI, na dawa zakulegeza misuli na kuambiwa afanye tiba ya akupankcha. Mgonjwa alipata nafuu ndani ya masaa mawili na kutokuwa na maumivu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 19:54:47
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.AANS.Cervical Spine. https://www.aans.org/en/Patients/Neurosurgical-Conditions-and-Treatments/Cervical-Spine. Imechukuliwa 17.11.2020
2.Levin K. Cervical spondylotic myelopathy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 17.11.2020
3.Radiculopathy. https://www.healthline.com/health/radiculopathy. Imechukuliwa 17.11.2020
4.Eubanks J. Cervical Radiculopathy: Nonoperative Management of Neck Pain and Radicular Symptoms. Am Fam Physician. 2010 Jan 1;81(1):33-40. Imechukuliwa 17.11.2020
5.Mila Nu Nu Htay etal. Cervical spondylosis mimicking cardiac angina. https://www.ijcrimedicine.com/archive/article-full-text/100050Z09MH2019#. Imechukuliwa 17.11.2020
6.Cervical Spondylosis.https://www.columbianeurology.org/neurology/staywell/cervical-spondylosis. Imechukuliwa 17.11.2020
7.Walter I. Sussman etal. Cervical Angina. An Overlooked Source of Noncardiac Chest Pain. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4272356/. Imechukuliwa 17.11.2020