Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya kiungulia cha pombe
7 Juni 2021 13:49:12
Utumiaji wa pombe huweza sababisha kupata kiungulia au watu wengi wakifahamu kama ngine chembe ya moyo. Hii ni kwa sababu kutumia pombe huambatana na tatizo la kucheua tindikali (GERD).
Matibabu yasiyo dawa
Matibabu ya kucheua tundikali au kiungulia kutokana na kunywa pombe yanahusisha kuacha pombe au kutumia pombe kwa mashariti yafuatayo;
Kunywa pombe kiasi kinachoshauri kiafya ambacho ni sawa na mililita 341 za bia yenye asilimia 5 au mililita 43 za vinyaji vikali kama vodika, kiroba n.k zeney asilimia 40 ya pombe au mililita 142 ya wine yenye asilimia 12 ya pombe. (kufahamu kuhusu kiasi cha pombe unatakiwa kunywa kiafya nenda kwenye Makala zingine ndani ya tovuti ya ulyclinic)
Usitumie pombe masaa 2 hadi 3 ya kuelekea muda wa kulala. Kulala kitandani baada ya kunywa husababisha kucheua pombe na tindikali zilizo tumbonina hivyo kukuletea dalili kali zaidi unapoamka.
Weka rekodi ya kila unachokula na kunywa ili utambue wakati gani au vyakula gani vimesabaisha upate dalili kali za kucheua tindikali. Achana na vitu vinavyokuletea kucheua tindikali zaidi endapo umeweza kuvitambua kwa rekodi ulizokuwa unaweka.
Angalia ni nini unachanganya na pombe, baadhi ya watu huweka limao kwa wingi au vinywaji vyenye carbon ambvyo husabaisha gesi tumboni na kuongeza uzalishaji wa tindikali. Zuia kuchanganya pombe na matunda au vinywaji vyenye tindikali kwa wingi ili kupunguza dalili za kucheua tindikali.
Kuacha kunywa pombe kabla ya kula chakula
Dawa za kuzuia kiungulia cha pombe
Dawa jamii ya PPI katika tafiti nyingi zimeonyesha kuwa hazina mwingiliano na pombe, wala pombe haizuii ufanyaji kazi wake, hivyo zinaweza kutumika pamoja na pombe. Licha ya kutumika pamoja ifahamike kwamba vinywaji vyenye kiwango kidogo cha pombe kama bia, huongeza uzalishaji zaidi wa tindikali na kuonekana zaidi kwa dalili za kiungulia, kichefuchefu n.k kwa wagonjwa waliotumia dawa za PPI na pombe, ukilinganisha na utumiaji vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha pombe kama wine, wiski, na vinginevyo.
Kundi la pili la dawa za kuzuia uzalishaji tindikali yaani H2 bloka (kama Famotidine, Cimetidine, Ranitidine na nizatidine) kwa sasa linahitaji zifanyiwe tafiti zaidi ili kuangalia kama kuna mwingiliano wenye mashiko wa kutumia dawa hizi na pombe.
Kumbuka
Endapo unataka kutumia dawa zilizoorodheshwa hapa chini, unashauriwa kutumia pombe kiasi kinachoshauriwa kutokana na mashariti yaliyoandikwa hapo juu. Ikiwezekana jipe muda wa nusu saa kabla ya kunjwa au saa moja baada ya kunywa pombe_
Dawa za PPI ni kama vile
Dawa za PPI zinazoweza kutumika kabla au baada ya kunywa pombe kwa ajili ya kiungulia ni;
Omeprazole
Esomeprazole
Lansoprazole
Dexlansoprazole
Pantoprazole
Rabeprazole