Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya kutostahimili laktosi
7 Juni 2021 13:53:31
Kutostahimili laktosi kwa jina la kiingereza lactose intolerance ni tatizo linalotokea endapo tumbo linashindwa kumeng’enya sukari ya laktosi inayopatikana kwenye maziwa au mazao ya maziwa. Tatizo hili hupelekea mtu kupata, maumivu ya chembe ya moyo (kiungulia), kuharisha na dalili zingine(soma kwa maelezo zaidi Makala hii sehemu nyingine kwenye tovuti ya ULY CLINIC).
Matibabu huhusisha kuepuka maziwa, kutumia maziwa yaliyopunguzwa au kutolewa kabisa laktosi au kutumia baadhi ya dawa ambazo huwa na kimeng’enya cha laktosi.
Dawa gani hutumika?
Dawa zinazotumika kuzuia kwa muda tatizo la kutostahimili laktosi ni;
Lactaid
Lactaid Ultra
Lactrase
Lactase
Surelac
Lactrol
Majina mengine ya dawa za kutostahimili kwa laktosi ni nini?
Dawa za kutostahimili kwa laktosi zinafahamika kama dawa za actose intolerance, dawa za kuharisha kutokana na kunywa maziwa, dawa za kuzuia kuharisha kutokana na maziwa, dawa za tumbo kujaa gesi kutokana na maziwa