Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za H.pylori
7 Juni 2021 14:05:46

Kuna dawa nyingi za kutibu vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya H.pylori. Matibabu ya H. Pylori mra nyingi huchukua takribani siku 14 hadi wiki 4(haswa dozi ya PPI) huendelezwa kwa muda mefu hadi wiki nane. Wasiliana na daktari wako siku zote ili kupata mchanganyiko sahihi wa dawa unaoendana na afya yako.
Nimchanganyiko gani hutumika kutibu H. Pylori?
Mchanganyiko huwa ni;
dawa moja ya PPI au HISTAMINE BLOKA
+
Mchanganyiko wa ANTIBAYOTIKI mbili
+
BISMUTH ( dawa ya kimiminika kama uji)
Dawa za PPI ni kama vile
Omeprazole
Esomeprazole
Lansoprazole
Dexlansoprazole
Pantoprazole
Rabeprazole
Dawa za H2 bloka ni kama vile
Famotidine (Pepcid AC,)
Cimetidine (Tagamet, Tagamet HB)
Ranitidine (Zantac, Zantac 75,)
Nizatidine tembe (Axid AR, Axid Capsules, Nizatidine tembe)
Machanganyiko wa dawa za antibayotiki zenye uwezo wa kuua H. pylori ni;
Metronidazole na tetracycline
Clarithromycin na amoxicillin
Clarithromycin na metronidazole
Clarithromycin na amoxicillin na Metronidazole
Levofloxacin na amoxicillin
Wapi unaweza pata taarifa zingine zaidi?
Soma zaidi kuhusu vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na H.pylori katika makala za uly clinic kisha wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyote ile.