Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kutibu maumivu ya koo
26 Machi 2021 11:45:57
Kwa sababu maumivu ya koo huweza kusababishwa na maambukizi ya bakteria, virusi au sababu za kimazingira na matumizi ya kemikali mbalimbali, katika Makala hii utajifunza dawa za kutibu maumivu ya koo katika makundi mbalimbali. Tafadhali rejea siku zote kupata maboresho ambayo yatafanyika kwenye dawa.
Dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye koo
Dawa jamii ya antibayotiki zinazotumika kwenye matibabu ya maambukizi ya koo yanayopelekea maumivu ya koo ni;
Azithromycin (Zithromax, Zmax, Z-Pak)
Cefixime (Suprax)
Cefuroxime (Ceftin)
Cephalexin (Keflex)
Clarithromycin (Biaxin)
Clindamycin (Cleocin)
Dawa za kupunguza maumivu ya koo na kuondoa dalili
Dawa hizi hupunguza au kuficha dalili ya maumivu ya koo lakini hazitibu kisababishi.
Dawa za maumivu
Acetaminophen (panado)
Ibuprofen
Aspirin (haipaswi kutumika kwa watoto na vijana wadogo)
Dawa za kuficha maumivu
Mucinex
Rhinase
Advil PM
Theraflu
Dawa ya kumumunya ya Tylenol
Dawa ya kupuliza kooni ya Chloraseptic
Dawa za kutibu maambukizi ya virusi wanaosababisha maumivu ya koo
Kwa sababu virusi huwa hawana dawa, matumizi ya dawa hizi hutumika kurudisha nyuma uzalianaji wa virusi vipya kooni na hivyo kupunguza dalili kwa kiasi kikubwa. Dawa hizi endapo zitatumika kabla ya maambukizi ya virusi huzuia kupata maumivu ya koo.
Rapivab (peramivir)
Relenza (zanamivir)
Tamiflu (oseltamivir)
Xofluza (baloxavir marboxil)
Dawa kupunguza maumivu ya koo kutokana na mzio(aleji)
Diphenhydramine
Fexofenadine
Loratadine
Pseudoephedrine
Oxymetazoline
Codeine
Hydrocodone
Dextromethorphan
Guaifenesin
Vitamin C
Taarifa zaidi kuhusu matibabu ya koo
Kupata taarifa zaidi kuhusu maumivu ya koo ingia kwenye kurasa zingine ndani ya tovuti hii kwa kutafuta kwenye kiboksi juu ya tovuti hii kilichoandikwa 'Tafuta chochote hapa....'