Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kutibu Trichomoniasis
7 Juni 2021 15:25:15
Ugonjwa huu husababisha na kimelea mwenye jina la Treponema vaginalis. Kwa sababu ni moja ya wa zinaa, matibabu yake huhusisha dawa za kutibu magonjwa ya zinaa, hata hivyo endapo maambukizi ya Treponema vaginalis yametambulika kwa vipimo.
Dawa za kutibu Trichomoniasis
Metronidazole au
Tinidazole
Kumbuka:
Matibabu yanatakiwa kuhusisha watu wote walioshiriki ngono yaani mtu na mpenzi au wapenzi wake. Endapo mtu mmoja atapata matibabu basi ni vema akaepuka kushiriki ngono na mpenzi wake au kutumia kondomu ipasavyo ili kuepuka kupata maambukizi mapya mpaka pale mpenzi wake atakapopata matibabu
Kila mtu anapswa kutumia dozi yake ni si kugawana dozi moja uliyoandikiwa na daktari
Majina mengine ya dawa za kutibu trichomoniasis
Baadhi ya watu wanatumia majina yafuatayo kumaanisha dawa za kutibu trichomoniasis
Dawa za kutibu uchafu sehemu ukeni
Dawa za kutoa harufu mbaya ukeni
Dawa ya kutoa harufu kama ya samaki ukeni
Dawa za kutibu uchafu wa njano ukeni
Dawa za kutibu uchafu wa kijani ukeni
Dawa za kutibu uke unaotoka na maji mengi yanayonuka
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Trichomoniasis
Soma zaidi kuhusu ugonjwa wa tricomoniasis katika makala zilizo kwenye tovuti ya uly clinic kwa kutafuta kwenye boksi la 'Tafuta chochote hapa...' juu ya tovuti hii.