Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kuzuia kucheua tindikali
7 Juni 2021 14:22:24
Kucheua tindikali husababishwa na kufunguka kwa koki inayozuia chakula kutoka tumboni kuja nje ya mwili kupitia mdomoni, tindikali zilizo tumboni hupanda juu na kuunguza umio pamoja na koo ambapo mtu hupata maumivu kwenye chembe ya moyo. Dawa zinazotumika kwenye matibabu ya tatizo la kucheua tindikali ni zile zinazpopunguza uzaishaji wa tindikali ambazo ni PPI au H2 BLOKA
Dawa aina ya PPI
Omeprazole
Esomeprazole
Lansoprazole
Dexlansoprazole
Pantoprazole
Rabeprazole
Dawa aina ya H2 bloka
Famotidine (Pepcid AC,)
Cimetidine (Tagamet, Tagamet HB)
Ranitidine (Zantac, Zantac 75,)
Nizatidine tembe (Axid AR, Axid Capsules, Nizatidine tembe)
Majina mengine ya dawa za kuzuia kucheua tindikali ni yapi?
Baadhi ya watu hutumia majina yafuatayo kumaanisha dawa za kuzuia kucheua tindikali, Dawa za GERD, dawa za kiungulia, dawa za maumivu katikati ya kifua, dawa za kuungua koo na tindikali n.k
Taarifa zaidi kuhusu kucheua tindikali unazipata wapi?
Ili kupata maarifa kuhusu tatizo la kuungua tindikali na endapo linafanana na kile ambacho unatafuta, ni vema ukasoma makala kuhusu kucheua tindikali ndani ya tovuti ya ULY CLINIC. Andika katika kiboksi cha Tafuta chochote hapa... juu ya tovuti hii ili kupata unachotaka soma.
Kumbuka
Kupata elimu zaidi kunafanya uwe na ujuzi na kisha kuondokana na ujinga, tunapenda wateja usome mwenyewe na kuelewa kisha kuwashilikisha wengine.