Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 18 Novemba 2021

Binzari
Binzari ni mmea unaoota aridhini na kutengeneza mizizi ambayo hutumika kama kiungo cha chakula na dawa. Mmea huu wenye asili ya India huwa na viuaji sumu kwa wingi na kemikali ya curcumin muhimu kwenye afya ya ubongo na mwili.
Virutubisho muhimu vinavyofanya kazi kama dawa ndani ya binzari hufyonzwa vema kama itatumika pamoja na pilipili manga.
Kuna aina nyingi za binzari lakini maarufu zaidi ni binzari ya manjano na binzari nyekundu.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye binzari
Mafuta
Protini
Nyuzilishe
Sukari
Madini
Vitamini
Kabohaidreti
Viinilishe vinavyopatikana kwenye binzari yenye ujazo wa gramu 100
Nishati = 312 Kilo kalori
Kabohaidreti = 67.14g
Mafuta = 3.25g
Protini = 9.68g
Nyuzilishe = 23g
Sukari = 3.2g
Maji = 12.85g
Madini yanayopatikana kwenye binzari yenye ujazo wa gramu 100
Kalishiamu = 168mg
Kopa = 1.3mg
Madini chuma = 55mg
Magineziamu = 208mg
Manganaizi = 19.8mg
Potashiamu = 2080mg
Fosifolasi = 299mg
Seleniamu = 6.2mg
Sodiamu = 27mg
Zinki = 4.5mg
Vitamini zinazopatikana kwenye binzari yenye ujazo wa gramu 100
Vitamini B1 = 0.058mg
Vitamini B2 = 0.150mg
Vitamini B3 = 1.350mg
Vitamini B5 = 0.542mg
Vitamini B6 = 0.107mg
Vitamini B9 = 20mg
Vitamini C = 0.7mg
Vitamini E = 4.43mg
Vitamini K = 13.4mg
Faida ya binzari kwenye mwili wa bianadamu
Huboresha afya ya ngozi
Hurekebisha kiwango cha suakri mwilini
Huondoa uchovu na kuupa mwili nguvu
Huondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
Huimarisha afya ya moyo, ngozi pamoja na ini
Huzuia kasi ya kupata ugonjwa wa kusahau pamoja na saratani
Huchangamsha mwili na kuondoa mawazo
Husaidia kupunguza uzito
Huimarisha mmeng`enyo wa chakula
Inapunguza athari ya ugonjwa wa baridi yabisi

Imeboreshwa,
18 Novemba 2021 16:03:57
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Vaughn, et al (2016). "effects of turmeric (curcuma longa) on skin health: a systematic review of the clinical evidence". Phytotherapy research. 30 (8): 1243–64.
Daily, et al (2016). "efficacy of turmeric extracts and curcumin for alleviating the symptoms of joint arthritis: a systematic review and meta-analysis of randomized clinical trials". Journal of medicinal food. 19 (8): 717–29.
Niir. board of consultants & engineers (2006). The complete book on spices & condiments (with cultivation, processing & uses). Delhi: asia pacific business press. Pp. 188–191. Isbn 9788178330389.
Imtiaz, et al(11 may 2016). "turmeric latte: the 'golden milk' with a cult following". The guardian. Imechukuliwa 18.11.2021
Health line. https://www.healthline.com/nutrition/top-10-evidence-based-health-benefits-of-turmeric#TOC_TITLE_HDR_3. Imechukuliwa 18.11.2021