Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Benjamin L, MD
Jumamosi, 4 Desemba 2021

Kitani
Mbegu za kitani ni mbegu zitokanazo na mmea wa kitani wenye asili ya ya mashariki ya kati, hata hivyo kwa sasa umeenea Duniani kote. Mbegu za kitani zimekua maarufu tangu enzi za kale kutokana na na na utajiri wa madini na vitamini zipatikanazo kwenye mbebgu hizi.
Viinilishe vya mbegu ya kitani
Kitani huwa na viinilishe vifuatavyo;
Protini
Kabohaidreti
Vitamini
Madini
Mafuta
Nyuzilishe
Viinilishe katika gramu 100 za kitani
Nishati = 534kcal
Kabohaidreti = 28.88g
Sukari = 1.55g
Mafuta = 42.16g
Omega 3 = 22.8g
Protini = 18.29g
Nyuzilishe =27.3g
Vitamini katika gramu 100 za kitani
Gramu 100 za kitani huwa na
Vitamini B1 = 1.644mg
Vitamini B2 = 0.161mg
Vitamini B5 = 0.985mg
Vitamini B6 = 0.473mg
Vitamini B9 = 87mcg
Madini katika gramu 100 za kitani
Gramu 100 za kitani huwa na;
Kalishiamu = 255mg
Madini Chuma = 5.73mg
Magineziamu = 392mg
Fosifolasi = 642mg
Potashiamu = 813mg
Zinki = 4.34mg
Faida za kitani
Kwa kula kitani unaweza kupata faida zifuatazo;
Kupunguza uzito
Kuimarisha afya ya moyo na kurekebisha shinikizo la damu
Kurekebisha na kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu
Kulainisha choo na kupunguza athari ya kupata choo kigumu
Kurekebisha kiwango kiwango cha sukari kwenye damu(inashauriwa kutumika sana kwa watu wenye tatizo la kisukari)
Kupunguza athari ya kupata saratani
Kupunguza athari ya kupatwa na magonjwa ya viungo
Kupunguza athari ya kupatwa na kansa ya mayai kwa wanawake
Kupunguza athari ya kupatwa na ugonjwa wa pumu
Majina mengine
Mbegu za kitani hufahamika pia kama;
Flax seed
Imeboreshwa,
4 Desemba 2021 16:53:48
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Kajla P., Sharma A., Sood D.R. Flaxseed-a potential functional food source. J. Food Sci. Technol. 2015;52:1857–1871.
Cressey P., Reeve J. Metabolism of cyanogenic glycosides: A review. Food Chem. Toxicol. 2019;125:225–232.
Hanif P.A., Gilani A.H. Dual effectiveness of flaxseed in constipation and diarrhea: possible mechanism. J. Ethnopharmacol. 2015;169:60–68.
Zhang X., Wang H., Yin P., Fan H., Sun L., Liu Y. Flaxseed oil ameliorates alcoholic liver disease via anti-inflammation and modulating gut microbiota in mice. Lipids Health Dis. 2017;16:44.
Parikh, Mihir et al. “Dietary Flaxseed as a Strategy for Improving Human Health.” Nutrients vol. 11,5 1171. 25 May. 2019, doi:10.3390/nu11051171