Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Dkt. Peter A, MD
Alhamisi, 16 Desemba 2021

Maziwa ya Hazeli
Yamesheheni kiasi kikubwa cha omega-3 na asidi nyingi zisizo na mafuta mengi na vitamin E Kuliko mimea mingine asili ya mbogamboga. Yana kiasi kidogo cha sukari kuliko maziwa mengine. Yamependekezwa kwa matukio ya kiungulia (umeng’enyaji dhaifu) na kisukari.
Maziwa asili ya mimea, pia hujulikana kwa jina la hortacha au ̏vinywaji vya msingi,̋ huwa mbadala wa kiafya wa maziwa ya ng’ombe kwa ajili ya watoto na watu wazima pia. Watoto wanaonyonya, ijapokuwa wanahitaji kutumia maziwa ya mama tu kwa angalau miezi sita ya uhai pasipo kinywaji kingine, wanaweza kutumia maziwa hata kama mbadala wa maziwa ya ng’ombe endapo maziwa maziwa ya mama hayapo au hayajitoshelezi.
Sifa za kawaida za maziwa yote ya asili ya mimea
Maziwa ya mchele huwa na;
Protini na sukari
Omega-3 na asidi nyingi zisizo na mafuta yaliyoshamiri
Vitamin E
Madini ya chuma (mengi kuliko kwenye maziwa ya ng’ombe), kiasi(kidogo kuliko kwenye maziwa ya ng’ombe), na madini mengine.
Maziwa ya mchele hupungukiwa;
Laktosi
Gluteni (protini ya wanga)
Lehemu
Vitamini B12
Imeboreshwa,
16 Desemba 2021 15:59:34
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Roselló-Soto, et al. “Enhancing Bioactive Antioxidants' Extraction from "Horchata de Chufa" By-Products.” Foods (Basel, Switzerland) vol. 7,10 161. 1 Oct. 2018, doi:10.3390/foods7100161