Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatano, 6 Mei 2020

Sumu kwenye chakula
Kudhuliwa na sumu ya chakula ni dalili zinazoonekana kutokana na kula chakula kilichochangamana na sumu ya bakteria, virusi, fangasi au kemikali za kiwandani au zinazozalishwa na vimelea.
Chakula kinaweza pata sumu wakati wa kuandaa kama mazingira ni machafu mfano mikono ya muadaaji, sehemu ya kuhifadhia chakula, chakula kimekaa muda gani, maji yanayotumika, vyombo vinavyotumika na hali ya kiafya ya muandaaji.
Dalili za mtu aliyedhuriwa na sumu ya chakula huanza kuonekana baada ya saa moja la kula.
Dalili ya kudhuriwa na sumu ya chakula
Dalili mara nyingi hutegemea na aina ya sumu iliyoliwa, baadhidi zinaweza kuwa;
Kichefuchefu
Kutapika
Kuhara maji au damu
Tumbo kuuma
Tumbo kuvuta
Homa
Dalili za hatari
Mara nyingi mtu akila sumu kwenye chakula, dalili huweza isha bila matibabu. Kama utapata dalili zifuatazo, onana na daktari mara moja;
Kutapika sana na mara kwa mara kiasi kwamba kitu hakibaki tumboni
Kutapika damu
Kuharisha kwa zaidi ya siku tatu
Maumivu makali ya tumbo au kubana kwa tumbo mara kwa mara
Joto la mwili kupanda
Dalili za kuishiwa maji mwilini kama kuwa na kiu sana, Kukauka midomo, kuishiwa nguvu, kukojoa kidogo au kutokujoa kabisa na kuhisi kizunguzungu
Kutokuona vizuri
Bakteria wanaotengeneza sumu kwenye chakula
Campylobacter
Clostridium botulinum
Clostridium perfringens
Escherichia coli (E. coli)
Giardia lamblia
Listeria
Noroviruses (Norwalk-like viruses)
Rotavirus
Salmonella
Shigella
Staphylococcus aureus
Makundi ya hatari zaidi kuathiriwa na sumu ya chakula
Wajawazito
Watu wazima
Watoto wadogo
Watu wenye magonjwa sugu
Kinga
Ili kujikinga na sumu ya chakula, fanya mambo yafuatayo;
Nawa mikono yako, osha vyombo vya chakula na safisha sehemu ambayo chakula knaandaliwa au kuhifadhiwa
Tenganisha vyakula ambavyo tayari vimeandaliwa na vile ambavyo havijaandaliwa
Pika chakula katika joto ambalo ni sahihi
Tunza vyakula kwenye jokofu katika hali ya ubaridi kuepuka kisiharibike
Usile vyakula vilivyoharibika au kukaa muda mrefu baada ya kupika endapo havijatunzwa sehemu sahihi
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:11:31
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
MayoClinic.FoodPoisoning.https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/food-poisoning/symptoms-causes/syc-20356230. Imechukuliwa 16/4/2020
HealthLine.FoodPoisoning.https://www.healthline.com/health/food-poisoning. Imechukuliwa 16/4/2020
MedicineNet.FoodPoisoning.https://www.medicinenet.com/food_poisoning/article.htm. Imechukuliwa 16/4/2020
Harrison Principles of Internal Medicine ISBN NI 9781259644030 Written by Tinsley R Harrison ukurasa wa 754