Mwandishi:
Mhariri:
Dkt.Peter R, CO
Dkt. Sospeter M, MD
Jumatatu, 13 Desemba 2021

Tufaa
Faida za tunda la Tufaa
Moyo na mishipa ya damu
Huwa na kemikali zenye uwezo wa kuzuia kutolewa kwa mafuta kutoka kwenye hifadhi yake na hivo huzuia mafuta kukusanyika katika damu ambayo ni kihatarishi cha magonjwa ya moyo na mishipa ya damu. Mafuta yanapojirundika katika mishipa ya damu huganda na kufanya izibe au kuwa na kipenyo kidogo, hali hii hupekekea kupanda kwa shinikizo la damu na magonjwa mengine mengi ya moyo na mishipa ya damu.
Tufaa pia huwa na vitamin C na hivyo huleta faida za vitamin hiyo.
Kudhibiti sukari katika damu
Katika mifumo tofauti , kemikali ya polyphenol iliyo ndani ya tufaha huweza kurekebisha umengenyaji wa chakula katika mfumo wa chakula na ndani ya chembe hai za mwili.
Kemikali ya Quercetin na zingine flavonoids hupunguza umengenyaji wa wanga na ufyonzwaji wa sukari baada ya kumengenywa
Tufaa huongeza utendaji kazi wa kongosho na hivo huzalisha kwa wingi homoni ya insulin inayopelekea kutumika na kupungua kwa sukari katika damu na kusababisha kuweka kiwango cha sukari kwenye hari nzuri
Tufaa pia husaidia kuongezeka kwa hisia ya chembe chembe zinazofyonza sukari na hivyo sukari hufayonzwa kutoka kwenye damu na kuingia kwenye chembechembe hizo na kudhibit sukari mwilini
Mbegu za tufaa pia huwa na vitamin B17 ambayo huweza kutumika kama dawa ya saratani ikitumiwa kwa usahihi.
Hivyo tufaa huwa na umuhimu katika mambo mengi sana katika mwili
Viinirishe vinavyopatikana kwenye tunda Tufaha
Mafuta
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Protini
Sukari
Madini
Vitamini
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Tufaha
Tunda la Tufaha lina kemikali muhimu ambazo ni hydroxybenzoic acid na hydroxycinnamic acid
Viinirishe vinavyopatikana kwenye tunda Tufaha
Nishati = 52kcl
Jumla ya mafuta = 0.2g
Sodiamu= 1mg
Sukari = 10g
Nyuzilishe = 2.4g
Protini = 0.3g
Kalishiamu= 6mg
Potashiamu =107mg
Madini chuma = 0.1mg
Madini yanayopatikana kwenye Tunda la Tufaha lenye Gramu 100
Chuma = 0.12mg
Kalishiamu = 6mg
Magineziamu = 5mg
Fosifolasi = 11mg
Potashiamu = 107
Sodiamu = 1mg
Floraidi = 3.3mg
Vitamini zinazopatikana kwenye Tunda la Tufaha lenye gramu 100
Vitamin A = 3mcg
Vitamini B1 = 0.017mg
Vitamini B2 = 0.026mg
Vitamini B3 = 0.091mg
Vitamini B5 = 0.061mg
Vitamini B6 =0.041mg
Vitamini B9 = 3mcg
Vitamini C = 4.6mg
Vitamini E = 0.18mg
Vitamini K = 2.2mcg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa tunda la Tufaha
Huimarisha kinga ya mwili
Huzuia ugonjwa wa kisukari
Huimarisha afya ya moyo na kuzuia shinikizo la juu la damu.
Huzuia kasi ya kupatwa na ugonjwa wa kansa
Huimarisha na kukukinga dhidi ya magonjwa ya Ini
Imeboreshwa,
28 Januari 2022 13:34:45
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Boyer, et al. “Apple phytochemicals and their health benefits.” Nutrition journal vol. 3 5. 12 May. 2004, doi:10.1186/1475-2891-3-5
Hyun, et al. “Apple as a source of dietary phytonutrients: an update on the potential health benefits of apple.” EXCLI journal vol. 15 565-569. 19 Sep. 2016, doi:10.17179/excli2016-483
Apple, nutritional value. https://www.nutritionvalue.org/Apples%2C_with_skin%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g. imechukuliwa 1. 12.2021.
Jensen GS, Attridge VL, Benson KF, Beaman JL, Carter SG, Ager D. Consumption of dried apple peel powder increases joint function and range of motion. J Med Food. 2014;17:1204–1213. Link
Kasai H, Fukada S, Yamaizumi Z, Sugie S, Mori H. Action of chlorogenic acid in vegetables and fruits as an inhibitor of 8-hydroxydeoxyguanosine formation in vitro and in a rat carcinogenesis model. Food Chem Toxicol. 2000 May;38(5):467-71. doi: 10.1016/s0278-6915(00)00014-4. PMID: 10762733. https://uc.xyz/163apw?pub=link. Imechukuliwa 1.12.2021
Qiao A, Wang Y, Xiang L, Wang C, He X. A novel triterpenoid isolated from apple functions as an anti-mammary tumor agent via a mitochondrial and caspase-independent apoptosis pathway. J Agric Food Chem. 2015;63:185–191.