Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatatu, 21 Machi 2022
Guacomole
Ni mchanganyiko unaopatikana baada ya kuchanganya parachichi, chumvi, sharubati ya ndimu na kitunguu maji ambapo hutumika kama kichanganyio kwenye chakula. Na imekua na faida nyingi kwa mwili wa mwanadamu.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Guacomole
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Guacomole
Guacomole ina kemikali mihumu ambazo ni oleic Acid.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Guacomole yenye gramu 100
Nishati = 167kcal
Mafuta = 13g
Kabohaidreti = 10g
Sukari = 3.3g
Nyuzilishe = 6.7g
Protini = 3.3g
Vitamini zinazopatikana kwenye Guacomole yenye gramu 100
Vitamini C =10mg
Madini yanayopatikana kwenye Guacomole yenye gramu 100
Madini Chuma = 1.2mg
Sodiamu = 433mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Guacomole
Huimarisha na kuboresha afya moyo Pamoja na kupunguza athari ya kupatwa na ugonjwa wa stroku
Huboresha afya nywele na Ngozi
Hupunguz uzito usiohitajika mwilini
Huongeza kinga ya mwili
Huimarisha afya ya macho na kuongeza uwezo wa kuona maradufu
Huzuia aina mbalimbali za kansa
Huboresha mfumo wa mmeng`enyo wa chakula
Huweka msawazo wa kiwango cha sukari pia kuzuia athari za ugonjwa wa kisukari
Huzuia kupatwa na ugonjwa wa tezi dume kwa wanaume
Huimarisha mifupa na kuzuia tatizo la urahisi wa kuvunjika kwa mifupa
Imeboreshwa,
21 Machi 2022, 16:15:11
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Trichopoulou A, Martinez-Gonzalez MA, Tong TY, Forouhi NG, Khandelwal S, Prabhakaran D, et al. . Definitions and potential health benefits of the mediterranean diet: views from experts around the world. BMC Med. (2014) 12:112. 10.1186/1741-7015-12-112. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7272688/. Imechukuliwa tarehe 13 January 2022.
Unlu NZ, Bohn T, Clinton SK, Schwartz SJ. Carotenoid absorption from salad and salsa by humans is enhanced by the addition of avocado or avocado oil. J Nutr. 2005 Mar;135(3):431-6. doi: 10.1093/jn/135.3.431. PMID: 15735074. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/15735074/. Imechukuliwa tarehe 13 January 2022.
https://www.nutritionvalue.org/Guacamole_598058_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 13 January 2022.