top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Benjamin L, MD

Ijumaa, 28 Januari 2022

Shelisheli
Shelisheli

Shelisheli ni tunda jamii ya fenesi lakini huwa na umbile dogo. Hupatikanakwenye kundi la matunda yanayotokana na miti ya maua kwenye familia ya Moraceae.


Shelisheli huwa na ladha kama ya kiazi kitamu na rangi yake huwa ya kupendeza macho.


Viinirishe vinavyopatikana kwenye Shelisheli


  • Mafuta

  • Kabohaidreti

  • Nyuzilishe

  • Protini

  • Sukari

  • Madini

  • Vitamini


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Shelisheli


Tunda la Shelisheli lina kemikali muhimu ziitwazo phenylalanine na leucine


Viinirishe vinavyopatikana kwenye Shelisheli


  • Nishati = 103kcl

  • Jumla ya mafuta = 0.2g

  • Kabohaidreti = 27mg

  • Sukari = 11g

  • Nyuzilishe = 4.9g

  • Protini = 1.1g

  • Maji = 70.65g


Madini yanayopatikana kwenye Tunda la Shelisheli lenye Gramu 100


  • Chuma = 0.54mg

  • Kalisiamu = 17mg

  • Magineziam = 25mg

  • Fosifolasi = 30mg

  • Potasiamu = 490mg

  • Sodiamu = 2mg

  • Zinki = 0.12mg


Vitamini zinazopatikana kwenye Tunda la Shelisheli lenye gramu 100


  • Vitamini B1 = 0.110mg

  • Vitamini B2 = 0.030mg

  • Vitamini B3 = 0.900mg

  • Vitamini B5 = 0.457mg

  • Vitamini B6 =0.1mg

  • Vitamini B9 = 14mcg

  • Vitamini C = 29mg

  • Vitamini E = 0.1mg

  • Vitamini K = 0.5mcg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa tunda la Shelisheli


  • Kupunguza maumivu ya viungo na misuli

  • Huzuia maambukizi ya bakteria

  • Hupunguza athari za kupatwa na ugonjwa wa kisukari

  • Huimarisha afya ya macho na kusaidia kuongeza uwezo wa kuona

  • Hulainisha haja kubwa

  • Husawazisha na kupunguza uzito mwilini


Majina mengine


Shelisheli hufahamika pia kwa lugha ya kiingeleza kama breadfruit

Imeboreshwa,
28 Januari 2022, 08:44:03
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Breadfruit nutritional value. https://www.nutritionvalue.org/Breadfruit%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa 20.12.2021.

  2. Liu Y, Ragone D, Murch SJ. Breadfruit (Artocarpus altilis): a source of high-quality protein for food security and novel food products. Amino Acids. 2015 Apr;47(4):847-56. doi: 10.1007/s00726-015-1914-4. Epub 2015 Jan 15. PMID: 25588988. 

  3. Ragone D. Breadfruit, Artocarpus altilis (Parkinson) Fosberg. Rome: International Plant Genetic Resources Institute; 1997. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7377419/#!po=0.505051.  Imechukuliwa  20.12. 2021.

bottom of page