Dalili za typhoid kwa mwanamke ni zipi?
Watu wengi wamekuwa wakiuliza kuhusu dalili za taifodi kwa wanawake. Makala hii imelenga kujibu swali hili.
Dalili za typhoid kwa mwanamke hazitofautiani na wanaume, mgonjwa anaweza mwenye maambukizi ya taifoid au parataifodi mara nyingi huwa na homa endelevu inayoanza taratibu na kuongezeka siku zinavyoenda bila kupungua na huweza kufika nyuzi joto za sentigredi 39 au 40 pamoja na dalili zifuatazo;
Uchovu mkali wa mwili
Maumivu ya kichwa
Kuharisha au haja ngumu
Kikohozi kikavu
Kutokwa na jasho
Kupoteza hamu ya kula
Kupoteza uzito
Mabaka kwenye ngozi yenye rangi ya ua waridi (Angalia picha)
Wakati gani uonane na daktari unapokuwa na dalili za taifodi?
Mwone daktari haraka iwezekanavyo unapohisi kuwa una dalili za taifodi kwa uchunguzi na tiba
Majina mengine ya dalili za typhoid kwa mwanamke
Majina mengine yanayotumika kumaanisha dalili za typhoid kwa mwanamke ni;
Dalili za taifodi kwa mwanamke
Dalili ya taifod kwa mwanamke
Dalili ya homa ya matumbo kwa wanawake
Rejea za mada hii;
CDC. Symptoms and Treatment. https://www.cdc.gov/typhoid-fever/symptoms.html. Imeandikwa 2.07.2021
Jameson JL, et al. Salmonellosis. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 20th ed. McGraw Hill; 2018. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imeandikwa 2.07.2021
Ryan ET. Epidemiology, microbiology, clinical manifestations, and diagnosis of typhoid fever. https://www.uptodate.com/contents/search. Imeandikwa 2.07.2021
ULY CLINIC taifodi