Kupata kinyesi chenye kamasi isikufanye uogope sana kwa kuwa mara nyingi ni hali ya kawaida. Kinyesi kwa kawaida kina kiwango kidogo cha kamasi ambacho husaidia kiweze kupita kirahisi kwenye utumbo mpana na kutoka nje.
Wakati gani wa kuhofia unapokuwa na kinyeshi chenye makamasi?
Unapaswa kuwa na wasiwasi endapo kinyesi chenye kamasi kimekuwa na sifa zifuatazo;
Kamasi kuwa nyingi zaidi ya kawaida
Kamasi kuwa na michirizi au matone ya damu
Kimeambatana na mabadiliko ya tabia ya tumbo kama maumivu ya tumbo n.k
Sababu gani zinaweza kusababisha kamasi kwenye kinyesi?
Kamasi kwenye kinyesi huweza sababishwa na;
Maambukizi mfumo wa umeng’enyaji chakula
Ugonjwa wa crohns
Ugonjwa wa asaletive kolaitiz
Saratani ya utumbo mpana
Kinyesi chenye kamasi kwa watoto
Visababishi vya kinyesi chenye kamasi kwa watoto vinaweza kuwa;
Sindromu ya iritabo baweli
Intusasepusheni
Asaletivu kolaitiz
Sistiki fibrosisi
Maambukizi tumboni ( amiba n.k)
Vidole kwenye utumbo
Mzio na chakula
Kutostahimili chakula
Kuharisha sana
Mabadiliko ya kunyonya maziwa
Rejea za mada hii;
Soma zaidi kwenye Makala ya ‘kinyesi chenye kamasi kwa mtoto’ na ‘kinyesi chenye kamasi kwa mtu mzima’ kwa uelewa zaidi.
LaRocque R, et al. Approach to the adult with acute diarrhea in resource-rich settings. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.06.2021
Stone CK, et al., eds. Pediatric emergencies. In: Current Diagnosis & Treatment: Emergency Medicine. 8th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2017. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 28.06.2021
Intussusception. https://pedclerk.bsd.uchicago.edu/page/intussusception. Imechukuliwa 28.06.2021
P Dutta, et al. Mucoid presentation of acute enterocolitis in children: a hospital-based case-control study. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10503679/. Imechukuliwa 28.06.2021
Zixiang Li,et al. Prospective Study on the Excretion of Mucous Stools and its Association with Age, Gender, and Feces Output in Captive Giant Pandas. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6562534/. Imechukuliwa 28.06.2021
Acid tumbon husababisha kinyesi chenye kamasi???
Video hii imeelezea kuhusu aina mbalimbali za vinyesi vya binadamu na maana yake kiafya
Kwa video mpya, subscribe kwenye youtube channel ya ULY CLINIC