Mazoezi ya mpangilio maalumu huwa na faidi nyingi kwa watu wealio na wasio na kisukari. Faidia za mazoezi kwa wagonjwa wa kisukari ni kuongeza ubora wa maisha, kuwapa nguvu, kuongeza mwitikio wa chembe hai kwenye insulin, kukinga magonjwa ya moyo na mishipa ya damu pamoja na madhara ya kisukari.
Licha ya kuwa na faida hizo, wagonjwa wa kisukari aina ya kwanza huweza kupata mabadiliko ya sukari kwenye damu yasiyo ya kawaida baada ya mazoezi..
Mazoezi ya nguvu kiasi kama vile kutembea, kuendesha baisklei, kukimbia taratibu na michezo mbalimbali hupunguza kiasi cha glukosi kwenye damu. Vivyo hivyo mazoezi ya nguvu nyingi zaidi kama mashindano ya riadha, kupiga mbio, kunyanyua vitu vyenye uzito mkubwa na yanayofanana na hayo husababisha ongezeko kupita kiasi la sukari kwenye damu wakati au baada ya kumaliza mazoezi.
Kwanini ongezeko la sukari kwenye damu wakati wakati wa mazoezi?
Kazi huongeza uwezo wa chembe hai kutumia glukosi iliyo kwenye damu, hivyo hivyo pia hutokea kwenye mazoezi. Mazoezi ya wastani au makali, huongeza uzalishaji wa homon msongo kwenye damu ambazo ni adrenalin na noradrenali. Homon hizo hucochea uzalishaji wa sukari kutoka kutoka kwenye glukagon (aina ya sukari iliyohifadhiwa na ini) ili kuufanya mwili utengeneze nguvu zaidi kwa mazoezi. Kiwango cha homon msongo huwa sambamba na kiwango cha mazoezi unayofanya, yanai endapo unafanya mazoezi makali, kiwango ch homon kitakuwa kikubwa.
Mazoezi ya wastani huambatana na ongezeko la glukagon lililo sambamba na kiwango cha insulin ili kuweka sawia kiwango cha glukosi. Mazoezi makali huongeza glukosi mara nane zaidi wakati insulin huongezeka mara tatu tu zaidi. Kukosekana kwa usawia wa ongezeko la glukosi na insulin, hupalekea kupanda kwa kiwango cha sukari wakati na baada tu ya kumaliza mazoezi.
Kwa kawaida, baada ya mazoezi makali, kiwango cha uzalishaji wa insulin huongezeka zaidi ili kuweka sawia kiwango cha glukosi kwenye damu, tendo hili hutokea kwa watu wenye afya na hushindikana kwa watu wenye kisukari.
Wagonjwa wa kisukari baada ya mazoezi makali, kiwango cha glukosi kwenye damu huzidi kuwa juu zaidi kwa sababu uzalishaji wa insulin huwa mdogo.
Naweza ugonjwa wa kisukari kutokana na mazoezi?
Kutokana na maelezo hapo juu, endapo mtu mwenye afya atafanya mazoezi na kujipima kisha kujikuta na kiwango cha juu cha sukari, hii haimaanishi kuwa ana tatizo bali ni hali ya kawaida inayoweza kutokea baada ya dakika kadhaa kufuatia mazoezi makali. Kiwango cha sukari kwenye damu hurejea kawaida baada ya dakika hadi masaa machache kupita. Kisukari cha mazoezi kwa wasio na kisukari huwa hakisababishi kupata ugonjwa wa kisukari.
Visababishi vya kupanda kwa kiasi cha sukari
Visababishi vya kisukari cha mazoezi huweza kuwa;
Kushindwa kuzalishwa kwa insulin ili kukabiliana na kiwango kikubwa cha homon adrenalin na noradrenalin baada ya mazoezi makali
Kula mlo mkubwa kabla ya mazoezi
Kupunguza dozi ya insulin kabla ya mazoezi
Kuna uwezekano wa kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu baada ya mazoezi?
Ndio, asilimia 30 ya wagonjwa wa kisukari cha kwanza wanaofanya mazoezi ya aerobiki ya wastani kwa muda wa dakika 45 mfululizo wakati wa jioni, kiwango cha sukari kwenye damu hupungua chini ya kiwango cha kawaida wakati wa usiku.
Nini cha kufanya kuzuia kisukari cha mazoezi kwa mgonjwa wa kisukari aina ya kwanza?
Njia rahisi ya kukabiliana na tatizo la kisukari cha mazoezi ni kuongeza kiwango cha wanga kabla ya mazoezi kulingana na kiwango cha sukari kwenye damu ulichopima kwenye mazoezi yaliyopita, kabla ya haya. Hata hivyo inaweza kuwa vigumu kufahamu ni kiasi gani cha wanga uongeze ili kuzuia kisukari cha mazoezi. Ukizingatia kwamba wanga wa ziada huongeza nishati zaidi mwilini, ili kuepuka hilo, njia nzuri zaidi inaweza kuwa kurekebisha kiasi cha insulin unachochoma kabla ya mazoezi.
Wapi utapata ushauri ushauri zaidi?
Kwa ushauri zaidi kuhusu kiasi gani cha wanga uongeze au urekebishe vipi kiasi cha insulin unachochoma, wasiliana na daktari wako. Unaweza pia kuwasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia kitufe cha 'mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii
Linki mbalimbali za maelezo ya kisukari
Kisukari na mambo yanayohusiana nayo. https://www.ulyclinic.com/kisukari-1
Visababishi vya kisukari. https://www.ulyclinic.com/vihatarishi-vya-kupata-kisukari-ain
Kitabu cha kisukari. https://www.ulyclinic.com/kisukari-2
Aina ya mazoezi ya kiafya. https://www.ulyclinic.com/aina-za-mazoezi
Mazoezi kwa wajawazito. https://www.ulyclinic.com/mazoezi-ya-uchungu-na-kujifungua
Mazoezi ya wagonjwa wa kisukari. https://www.ulyclinic.com/kisukari-2/Mazoezi-kwa-wagonjwa-wa-kisukari
Chakula na mazoezi. https://www.ulyclinic.com/program-ya-mazoezi
Majina mengine ya Makala hii
Makala hii imejibu maswali yafuatayo;
Ongezeko la sukari mwilini baada ya mazoezi
Mazoezi husababisha kisukari?
Kisukari baada ya mazoezi
Kumbuka
Neno glukosi katika makala hii limetumika kama mbadala wa neno sukari na humaanisha sukari inayotumiwa na chembe hai ili kupata nguvu, inayopimwa pia kwenye kipimo cha glukometa.
Rejea za mada hii
R. M. Bracken, et al. Exercise-induced hyperglycaemia in the absence of diabetes. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/full/10.1111/j.1464-5491.2010.02960.x. Imechukuliwa 12.07.2021
Dessi P. Zaharieva, et al. Prevention of Exercise-Associated Dysglycemia: A Case Study–Based Approach. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4334080/.Imechukuliwa 12.07.2021
Galassetti P, Riddell MC. Exercise and type 1 diabetes (T1DM). Compr Physiol 2013;3:1309–1336
Riddell M. The impact of type 1 diabetes on the physiological responses to exercise. In Type 1 Diabetes. Gallen I, Ed. London, Verlag, 2012, p. 29–45
Sigal RJ, Purdon C, Fisher SJ, Halter JB, Vranic M, Marliss EB. Hyperinsulinemia prevents prolonged hyperglycemia after intense exercise in insulin-dependent diabetic subjects. J Clin Endocrinol Metab 1994;79:1049–1057
Fahey AJ, et al. The effect of a short sprint on postexercise whole-body glucose production and utilization rates in individuals with type 1 diabetes mellitus. J Clin Endocrinol Metab 2012;97:4193–4200
Koivisto VA, et al. Postprandial blood glucose response to exercise in type I diabetes: comparison between pump and injection therapy. Diabetes Care 1983;6:436–440 [PubMed] [Google Scholar]
Rabasa-Lhoret R, et al. Guidelines for premeal insulin dose reduction for postprandial exercise of different intensities and durations in type 1 diabetic subjects treated intensively with a basal-bolus insulin regimen (ultralente-lispro). Diabetes Care 2001;24:625–630
Campbell MD, et al. . Large pre- and postexercise rapid-acting insulin reductions preserve glycemia and prevent early- but not late-onset hypoglycemia in patients with type 1 diabetes. Diabetes Care 2013;36:2217–2224
Delvecchio M, et al. Effects of moderate-severe exercise on blood glucose in type 1 diabetic adolescents treated with insulin pump or glargine insulin. J Endocrinol Invest 2009;32:519–524
Tsalikian E, et al. Prevention of hypoglycemia during exercise in children with type 1 diabetes by suspending basal insulin. Diabetes Care 2006;29:2200–2204 [PMC free article] [PubMed] [Google Scholar]
LaMonte MJ, et al. Physical activity and diabetes prevention. J Appl Physiol 2005; 99: 1205– 1213.
Hirsch IB, et al.Insulin and glucagon in prevention of hypoglycemia during exercise in humans. Am J Physiol 1991; 260: E695– E704.
Wasserman DH, et al. Glucagon is a primary controller of hepatic glycogenolysis and gluconeogenesis during muscular work. Am J Physiol 1989; 257: E108– E117.
Marliss EB, et al. Glucose turnover and its regulation during intense exercise and recovery in normal male subjects. Clin Invest Med 1992; 15: 406– 419.
Marliss EB, et al. Intense exercise has unique effects on both insulin release and its roles in glucoregulation: implications for diabetes. Diabetes 2002; 51 (Suppl. 1): S271– S283.
Goodyear LJ, et al. Exercise-induced translocation of skeletal muscle glucose transporters. Am J Physiol 1991; 261: E795– E799.
Marliss EB, et al. Glucoregulatory and hormonal responses to repeated bouts of intense exercise in normal male subjects. J Appl Physiol 1991; 71: 924– 933.