Kama una muwasho wa pumbu au ngozi ya korodoni na maeneo ya kinena, ni vema ukawasiliana na daktari ili akusaidie kufahamu shida yako inasababishwa na nini haswa baada ya kuulizwa maswali ya kitaalamu kisha kutapatiwa matibabu kulingana na shida yako.
Visababishi vya muwasho wa pumbu na kinena
Wengi wamekuwa wakidhani kuwa muwasho wa pumbu au ngozi ya korodani na maeneo ya kinena husababishwa na maambukizi ya fangasi tu, hii si sahihi kwa kuwa kuna sababu lukuki zinazoweza pelekea muwasho wa maeneo haya. Endapo una tatizo la muwasho, tafadhali wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi.
Muwasho kwenye pumbu na kinena unaweza sababishwa na;
Fanya ngozi yako iwe na unyevu kwa kuogea sabuni au kupaka mafuta yanayoongeza unyevu kama muwashounasababishwa na ukavu wa ngozi
Tumia sabuni za kuogea zenye zinki, selenium sulfide au ketoconazole kama unahisi una maambukizi ya fangasi
Punguza msongo wa mawazo na msongo wa mwilini. Njia kama kupumzisha akili, kufanya mazoezi, kuwa na tafakuri ya kina, huweza kupunguza msongo wa mawazo kwa baadhi ya watu.
Tumia dawa zisizohitaji cheti zinazozuia mzio kama dawa ya diphenhydramine na krimu ya hydrocortisone
Zuia kujikuna ngozi yako, kama unajikuna ukiwa usingizini, kata kucha zako na ikiwezekana funika eneo lilalowasha ili kuzuia kujikuna kunakoweza pelekea majeraha na maambukizi kwenye eneo lilalowasha.
Oga au safisha eneo linalowsha kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye magadi soda. Hii husaidia kupunguza muwasho wa pumbu
Pata muda wa kupumzika na kulala. Hii hupunguza vihatarishi vya mwili wako kuwasha
Majibu hayo juu yanajibu maswali mengine kama dawa ya vipele na muwasho sehemu za siri, dawa ya kujikuna sehemu za siri, dawa ya muwasho wa ngozi, dawa ya mzio wa ngozi, dawa za kuwashwa mwili.
Ushauri muhimu kwa wanaowashwa pumbu
Kama una muwasho wa pumbu au ngozi ya korodoni na maeneo ya kinena, ni vema ukawasiliana na daktari ili akusaidie kufahamu shida yako inasababishwa na nini haswa baada ya kuulizwa maswali ya kitaalamu kisha kutapatiwa matibabu kulingana na shida yako.
Visababishi vya muwasho wa pumbu na kinena
Wengi wamekuwa wakidhani kuwa muwasho wa pumbu au ngozi ya korodani na maeneo ya kinena husababishwa na maambukizi ya fangasi tu, hii si sahihi kwa kuwa kuna sababu lukuki zinazoweza pelekea muwasho wa maeneo haya. Endapo una tatizo la muwasho, tafadhali wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi.
Muwasho kwenye pumbu na kinena unaweza sababishwa na;
Mzio (allergy)
Pumu ya ngozi
Chawa wa kwenye maeneo ya siri
Chunjua kwenye pumbu
Kisonono
Maambukizi ya chlamydia
Maambukizi ya kirusi cha herpes
Maambukizi ya fangasi kwenye pumbu na kinena
Misuguano ya pumbu kutokana na ukavu
Ugonjwa wa skabi
Ugonjwa wa trikomoniasis
Baadhi ya dawa za kuondoa muwasho lakini hazitibu kisababishi cha muwasho wa pumbu zimeorodheshwa hapa chini.
Dawa zenye uwezo wa kutuliza muwasho wa pumbu
Krimu ya Hydrocortisone
Diphenhydramine
Benzocaine
Capsaicin
Triamcinolone
Doxepin
Fluoxetine
Sertraline
Kumbuka dawa hizo huficha tu dalili ya muwasho lakini hazitibu kisababishi, isipokuwa endapo kisababishi ni magonjwa ya mzio.
Endapo unataka tiba ya tatizo lako itabidi uwasiliane na daktari kwa uchunguzi zaidi.
Matibabu ya nyumbani ya kuwashwa na pumbu au sehemu nyingine ya mwili
Epuka kutumia vitu vinavyosababisha uwashwe. Jaribu kutambua vitu vinavyosababisha muwasho kwako kisha kuviacha.
Fanya ngozi yako iwe na unyevu kwa kuogea sabuni au kupaka mafuta yanayoongeza unyevu kama muwashounasababishwa na ukavu wa ngozi
Tumia sabuni za kuogea zenye zinki, selenium sulfide au ketoconazole kama unahisi una maambukizi ya fangasi
Punguza msongo wa mawazo na msongo wa mwilini. Njia kama kupumzisha akili, kufanya mazoezi, kuwa na tafakuri ya kina, huweza kupunguza msongo wa mawazo kwa baadhi ya watu.
Tumia dawa zisizohitaji cheti zinazozuia mzio kama dawa ya diphenhydramine na krimu ya hydrocortisone
Zuia kujikuna ngozi yako, kama unajikuna ukiwa usingizini, kata kucha zako na ikiwezekana funika eneo lilalowasha ili kuzuia kujikuna kunakoweza pelekea majeraha na maambukizi kwenye eneo lilalowasha.
Oga au safisha eneo linalowsha kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye magadi soda. Hii husaidia kupunguza muwasho wa pumbu
Pata muda wa kupumzika na kulala. Hii hupunguza vihatarishi vya mwili wako kuwasha
Soma zaidi kuhusu visababishi vya muwasho wa ngozi baada ya kuoga na matibabu yake
Soma kuhusu fangasi kwenye pumbu na matibabu yake kwa kubofya maandishi ya kijani yaliyokolezwa
Kwa maswali zaidi unaweza kuuliza kupitia email au kupitia forum hii ya ULY CLINIC na utajibiwa na wataalamu wa afya wa ULY CLINIC
Rejea za mada hii
A Krishnan, et al. Scrotal Dermatitis - Can we Consider it as a Separate Entity?. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3769120/. Imechukuliwa 22.06.2021
U Wollina. Red scrotum syndrome https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3184780/. Imechukuliwa 22.06.2021
American Family Physician. Pruritus. https://www.aafp.org/afp/2003/0915/p1135.html. Imechukuliwa 22.06.2021
Tinea cruris. Tanzania standard treatment guideline toleo la 2021
Healthline. Scrotal Eczema. https://www.healthline.com/health/scrotal-eczema. Imechukuliwa 22.06.2021