Itachukua siku ngapi kutambua nina UKIMWI bila kupima?
Dalili za UKIMWI huonekana baada ya siku ngapi?
Itachukua siku ngapi kutambua nina HIV bila kupima?
Inachukua siku ngapi kujitambua nina maambukizi ya virusi vya UKIMWI bila kupima?
Nitatamtabuaje mtu mwenye UKIMWI bila kupima?
Ninawezaje kumtambua mwathirika wa VVU?
top of page
To see this working, head to your live site.
Natambuaje UKIMWI bila kupima?
Natambuaje UKIMWI bila kupima?
1 answer0 replies
Like
Maoni (1)
bottom of page
Hayo ni maswali watu wengi wamekuwa wakiuliza na yamejibiwa kwenye Makala hii fupi
Ni muhimu ufahamu kwanza?
Maswali yote yamelenga kuuliza namna ya kutambua maambukizi ya VVU/ UKIMWI bila kupima. Hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya nyakati kwa sababu kuna maambukizi mengine ambayo yanaweza kuleta dalili zinazofanana na dalili za mwanzo za UKIMWI, mfano maambukizi ya virusi wengine kama kirusi cha mafua (influenza), UVIKO-19 au corona n.k
Endapo unahisi umepata maambukizi ya VVU njia pekee ya kutambua ni kwa kupima naam hata kama upo hatua za mwisho, kwa sababu unaweza kuwa na ugonjwa wowote ule unaoleta dalili kama za UKIMWI. Endapo utapima na kutambulika mapema na kuanza dawa, utadhibiti dalili nyingi na kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine wasio na maambukizi.
Je inachukua siku ngapi kuanza kuona dalili za ukimwi pasipo kupima?
Swali hili linajibiwa vema kwa kutumia dalili za kila hatua za maambukizi ya Virusi vya UKIMWI
Hatua ya kwanza ya maambukizi ya VVU
Hatua ya kwanza huambatana na dalili ambazo hutokea kwa kipindi cha ndani ya siku 14 hadi 28 baada ya kupata maambukizi na hudumu kwa siku au wiki chache.
Homan na kutetemeka
Kutokwa jasho wakati wa usiku
Kuvimba tezi limfu
Maumivu ya misuli
Kukauka kwa koo
Harara kwenye ngozi au vipele
Uchovu mkali
Vidonda ndani ya kinywa
Dalili hizi huonekana chini ya asilimia 70 ya walioapata VVU
Hatua ya pili ya maambukizi ya VVU
Unaweza kupita hatua ya kwanza bila kutambua una VVU kwa sababu hujapata dalili na kuingia kwenye hatua hii ya pili.
Ni dalili gani huonekana kwenye hatua ya pili?
Hatua ya pili inaweza kuchukua kipindi cha miaka 10 hadi 15, na huwa haina dalili yoyote hasa katika hatua za awali. VVU huzaliana kwa wingi na kuharibu mfumo wa kinga ya mwili inayopelekea kuingia hatua ya tatu. Kwenye hatua ya pili karibia na kuingia hatua ya tatu dalili zifuatazo zinaweza kuonekana kwa kiasi kidogo tu;
Kupoteza uzito bila sababu chini ya asilimia 10 ya uzito wa mwanzo
Maambukizi ya mfumo wa upumuaji kama sinusaitizi, kupata matezi n.k
Kama mkanda wa jeshi
Kupasuka pembe za midomo
Vidonda vya mara kwa mara kwenye pembe za midomo
Kuzuka kwa upele mwili mzima unaowasha wenye rangi ya zambarau
Fangasi wa kwenye vidole
Magonjwa mengine ya ngozi
Hatua ya tatu ya maambukizi ya VVU
Hatua ya tatu ni kuonekana kwa dalili za Upungufu wa Kinga MWilini yaani UKIMWI, hatua hii huonekana miaka 10 au 15 baada ya kupata maambukizi ya VVU bila kupata tiba. Dalili zinazoonekana kwenye hatua ya tatu ya maambukizi ya VVU ni matokeo ya kuharibiwa kwa mfumo wa kinga ya mwili. Maradhi mbalimbali humpata mwathirika kwa sababu kinga ya mwili kushindwa kumlinda mwathirika dhidi ya maambukizi mbalimbali. Dalili za hatua ya tatu ya UKIMWI zinajumuisha;
Kupoteza uzito kwa kasi
Homa za mara kwa mara
Kutokwa jasho jingi wakati wa usiku
Kuchoka sana mwili kusiko na sababu muhimu
Kuvimba kwa tezi limfu kwenye shingo, kwapa na maeneo ya kinena
Kuharisha kwa muda mrefu na kwa kujirudia rudia
Kuugua magonjwa ya mfumo wa mapafu kama nimonia
Vidonda kwenye midomo, na maeneo ya haja kubwa
Kupoteza uzito zaidi ya asilimia 10 ya uzito wa awali
Kupotezakumbukumbu, mdongo wa mawazo
Dalili zingine za uharibifu wa mfumo wa neva
Hatua ya nne ya UKIMWI
Hii ni hatua mbapo mgonjwa anapata dalili kali zaidi ya zile za hatua ya tatu na hata kupata saratani. Hatua hii huchukua miezi michache kabla ya mgonjwa kupatwa na umauti hata akianza dawa za ART, endapo atafanikiwa kuishi ndani ya mwaka mmoja wa kwanza, asilimia 95 ya wagonjwa hufa ndani ya miaka mitano. Dalili hizo ni;
Kukonda sana kiasi cha kuonekana kwa mifupa
Nimonia ya PCP
Nimonia ya kujirudia rudia
Kifua kikuu cha nje ya mapafu
Maambukizi ya toxoplasmosis
Saratani ya kaposis(Kuota upele mgumu wenye rangi ya pinki, kahawia au zambarau maeneo mbalimbali ya mwili)
Maambukizi ya fangasi kwenye umio
Fistula
Saratani ya tezi limfu
Na magonjwa mengine
Rejea za mada hii
HV. Gov. Symptoms of HIV. https://www.hiv.gov/hiv-basics/overview/about-hiv-and-aids/symptoms-of-hiv. Imechukuliwa 21.06.2021
Jennifer L. Weinberg, et al. The WHO Clinical Staging System for HIV/AIDS. https://journalofethics.ama-assn.org/article/who-clinical-staging-system-hivaids/2010-03#. Imechukuliwa 21.06.2021
INTERIM WHO CLINICAL STAGING OF HIV/AIDS AND HIV/AIDS CASE DEFINITIONS FOR SURVEILLANCE. https://www.who.int/hiv/pub/guidelines/clinicalstaging.pdf. Imechukuliwa 21.06.2021
Aids Map. The stages of HIV infection. https://www.aidsmap.com/about-hiv/stages-hiv-infection. Imechukuliwa 21.06.2021
Tanzania standard treatment guideline (STG) toleo la 2021