top of page
To see this working, head to your live site.
Nawezaje kufahamu tarehe yangu ya kujifungua endapo nimesahau tarehe ya mwisho kuona damu ya hedhi?
Nawezaje kufahamu tarehe yangu ya kujifungua endapo nimesahau tarehe ya mwisho kuona damu ya hedhi?
1 answer0 replies
Like
Maoni (1)
bottom of page
Unawezaje kufahamu tarehe yako ya kujifungua?
Mwanamke anatakiwa kujua tarehe yake ya kujifungua ili aweze kujiandaa, hata hivyo ni muhimu sana wewe na mpenzi wako kufahamu ni lini unatarajia kupata mtoto ili kutoa muda wa kufanya maandalizi ya kifedha na namna ya kujifungua.
Endapo umesahau tarehe yako ya kwanza mara ya mwisho kuona damu ya hedhi, unaweza kukisia tarehe hiyo kwamba ilikuwa ni mwanzoni, katikati au mwishoni mwa mwezi kisha kuweka tarehe hiyo kwenye kikokoteo cha tarehe ya kujifungua chini ya makala hii. Kumbuka endapo ulisahau tarehe yako ya mwanzo kuona damu ya hedhi njia hii inakuwa si sahihi zaidi.
Njia nyingine unaweza kuitumia ni kwa kupimwa ukubwa wa tumbo lako la uzazi ili kujua umri wa mimba na tarehe ya kujifungua au kutumia kipimo cha ultrasound ambacho huwa sahihi zaidi haswa kwenye ujauzito wenye umri chini ya miezi minne.
Bonyeza hapa kusoma zaidi au kutumia kikokoteo kufahamu tarehe ya kujifungua