Mishipa inayozubguka mlango wa kutolea kinyesi(mkundu) hutanuka kukiwa na shinikizo kubwa/ mgandamizo na hivo huweza kujaa au kuvimba kutokana na kuwepo kwa damu ndani yake. Mishipa iliyovimba maeneo haya huitwa hemorrhoids hutokea na vitu vifuatavyo vinaweza kuongeza shinikizo maeneo hayo kisha kusababisha mishipa hii kuvimba
Kukenya wakati wa kujisaidia (kutumia nguvu nyingi wakati wa kutoa haja kubwa
Kukaa mda mrefu chooni unapokuwa unajisaidia
Kuhara kwa muda mrefu au choo kigumu
Kitumbo(kuwa na tumbo kubwa) uzito kupita kiasi
Ujauzito
Kufanya mapenzi kwa njia ya haja kubwa-Kulawiti
Kula chakula chenye nyuzinyuzi kidogo
Bawasili hutokea sana kwa watu wazima au wanaapokuwa wazee maana kuta zinazozuia mishipa hii huvutika na kutanuka jinsi mtu anavyokuwa mzee