Rangi ya kawaida ya kinyesi cha mtoto ni ipi?
Rangi isiyo ya kawaida ya kinyesi cha mtoto ni ipi?
Ni wakati gani wa kuhofia rangi ya kinyesi cha mtoto inapobadilika?
Rangi ya kinyesi cha mtoto na maana yake
top of page
To see this working, head to your live site.
Rangi ya kinyesi cha mtoto
Rangi ya kinyesi cha mtoto
2 answers0 replies
Like
Maoni (2)
bottom of page
Rangi ya kinyesi cha kawaida kwa mtoto
Rangi ya kinyesi cha kawaida kwa watoto hutegemea umri na anachokula. Makala hii imeelezea kwa ufupi kuhusu rangi mbalimbali za kawaida na zisizo za kawaida
Rangi nyeusi au kijani iliyokolea
Ni rangi ya kawaida ya kinyesi kwa kichanga mara baada ya kuzaliwa na hufahamika kama mekoniamu. Mekoniamu ni kinyesi cha kwanza cha kichanga na huweza kudumu kwa muda wa siku 2 au zaidi ikitegemea hali ya unyonyaji wa mtoto.
Rangi ya njano inayoelekea kijani
Ni rangi ya kawaida kwa mtoto anapoanza kunyonya. Kinyesi cheusi cha kwanza hubadilika kuwa cha njano inayoelekea kijani na hiki hudumu kwa siku chache kabla ya kuja kinyesi cha njano.
Rangi ya njano
Rangi ya njano hufahamika na watu wengi watu wengi kuwa ni kinyesi cha kawaida na hufuata baada ya kuonekana kinyesi cha njano kuelekea kijani. Kinyesi cha njano huendelea kwa muda mrefu mpaka pale mtoto atakapoanza kula vyakula vingine mbali na maziwa ya mama au maziwa ya kopo.
Rangi ya kahawia iliyopauka au njano
Kwa watoto wanaotumia maziwa ya kopo au wanaonyonya maziwa ya mama ni kawaida kuwa na kinyesi cha rangi ya kahawia au njano.
Rangi ya kahawia iliyopauka , njano au kijani
Kinyesi rangi hii ni kawaida kwa watoto wanaotumia maziwa ya kopo tu
Rangi ya kinyesi baada ya kuanza changanyiwa chakula(baada ya miezi sita)
Mtoto anapoanza kula vyakula vingine, yaani aada ya kuvuka miezi sita hupata rangi nyingine nyingi zaidi kama kijani, nyekundu, n.k ikitegemea chakula alichokula. Kitu cha muhimu ni kutambua nini alichokula mtoto kabla ya kusema rangi hiyo ni kawaida au sio.
Rangi gani za kinyesi si za kawaida?
Mtoto akianza kupata kinyesi cha rangi zifuatazo unapaswa kuhofu na kutafuta msaada wa daktari haraka kwa uchunguzi;
Kinyesi chenye damu nyekundu au kuwa cheusi na kunata baada ya kuanza kupata kinyesi cha kijani
Kinyesi kilichopauka (cheupe) au chenye rangi ya kijivu
Kuhara (anaharisha zaidi ya mara tatu kwa siku)
Kinyesi kigumu zaidi mpaka kupata shida wakati wa kujisaidia
Kinyesi chenye mrenda na kutoa harufu kwa watoto ambao wameshaanza kula vyakula vya familia
Wapi unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu rangi ya kiyesi na maana yake kiafya?
Pata taarifa zaidi kuhusu rangi ya kinyesi cha mtoto kwa kutafuta kila rangi kwenye makala za ulyclinic. mfano tafuta 'kinyesi cha kijani' au kwa kubofya hapa
Rejea za mada hii;
Jolanda den Hertog , et al. The defecation pattern of healthy term infants up to the age of 3 months. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/22522220/. Imechukuliwa 21.06.2021
Jennifer Gustin BS, et al. Characterizing Exclusively Breastfed Infant Stool via a Novel Infant Stool Scale. https://aspenjournals.onlinelibrary.wiley.com/doi/10.1002/jpen.1468. Imechukuliwa 21.06.2021
Health children. org. Baby’s first bowel movements. healthychildren.org/English/ages-stages/baby/diapers-clothing/Pages/Babys-First-Bowel-Movements.aspx. Imechukuliwa 21.06.2021
Health children. org. Baby's first days: Bowel movements & urination. healthychildren.org/English/ages-stages/baby/Pages/Babys-First-Days-Bowel-Movements-and-Urination.aspx. Imechukuliwa 21.06.2021
Mayoclinic. I'm breast-feeding my newborn and her bowel movements are yellow and mushy. Is this normal for baby poop?. mayoclinic.org/healthy-lifestyle/infant-and-toddler-health/expert-answers/baby-poop/faq-20057971. Imechukuliwa 21.06.2021
How to treat diarrhea in infants and young children. fda.gov/consumers/consumer-updates/how-treat-diarrhea-infants-and-young-children. Imechukuliwa 21.06.2021
Johns Hopkins Medicine. The color of poop: Stool guide, mobile app to speed up diagnoses of life-threatening liver condition in newborns [Press release]. hopkinsmedicine.org/news/media/releases/the_color_of_poop_stool_guide_mobile_app_to_speed_up_diagnoses_of_life_threatening_liver_condition_in_newborns. Imechukuliwa 21.06.2021
Health children. org. The many colors of poop. healthychildren.org/English/ages-stages/baby/Pages/The-Many-Colors-of-Poop.aspx. Imechukuliwa 21.06.2021
Health children. org . Pooping by the numbers. healthychildren.org/English/ages-stages/baby/Pages/Pooping-By-the-Numbers.aspx. Imechukuliwa 21.06.2021
Hopkins medicine. What can your child's poop color tell you? (n.d.). hopkinsmedicine.org/johns-hopkins-childrens-center/what-we-treat/specialties/gastroenterology-hepatology-nutrition/stool-color-overview.html. Imechukuliwa 21.06.2021