Naomba kufahamu visababishi vya presha kwa mjamzito ?
Sababu za presha kwa mjamzito na tiba yake ni nini?
top of page
To see this working, head to your live site.
Edited: Jul 26, 2021
Visababishi vya presha kwa mjamzito
Visababishi vya presha kwa mjamzito
1 answer0 replies
Like
Maoni (1)
bottom of page
Kuna matatizo mengi ya presha yanayofahamika na huweza kutokea wakatiwa ujzuzito, matatizo hayo ni pamoja na Shinikizo la juu la damu lililo sugu, shinikizo la juu la damu linaloeekea kifafa cha mimba, kifafa cha mimba (eclampsia) na shinikizo la juu la damu la ujauzito(gestational hypertension). Matatizo haya yote ni hatari kwa mama na mtoto. Utambuzi wa mapema huweza kufanyika endapo mama ana hudhuria kliniki.
Vihatarishi
Vihatarishi vya kupatashinikizo la juu la damu ni pamoja na hali mbalimbali zinazopunguza mzunguko wa damu kati ya mfuko wa uzazi na kitovu cha mtoto pamoja na Kutojimudu kwa mishipa ya damu kutokana na matatizo yaliyopo kama shinikizo la damu kabla ya ujauzito(shinikizo sugu la damu), magonjwa ya figo, kisukari, ugonjwa wa thrombophilia na magonjwa mengine ya shambulio la mfumo wa kinga huongeza hatariya kupata shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito
Vihatarishi vinginine ni vinavyoongeza hatari kuwa ya kupata shinikizo la juu la damu kwenye ujauzito ni;
Kuwa na historia ya Shinikizo la damu linaloelekea kufafa cha mimba, kuwa na historia ya Sindromu ya HELLP, kuwa na historia ya kupata mapacha au watoto zaidi ya wawili kwenye mimba moja, kuwa na BMI zaidi ya 30(ugonjwa wa obeziti), kuwa na ujauzito wa kwanza na kuwa na historia kwenye familia ya ndugu wa damu moja kuwa na tatizo la kifafa cha mimba
Visababshi
wanasayansi bado hawajaelewa vema Pathophysiologia ya shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito. Tafiti mpya zimeonyesha kuwa, madhaifu katika hatua za ujauzito haswa kipindi cha mwanzo ambapo yai lililochavushwa linajishikiza kwenye ukuta wa uzazi, kuna kemikali mbalimbali zinazotolewa zenye majina ya cytokine, molecule za ushikizaji, molecule za histocompatibility complex na metalloproteinases ambazo huhusika kwa asilimia kubwa kusababisha shinikizo la juu la damu. Kemikali hizi zinapozaliswha kwa wingi husababisha madhaifu katika utengenezaji wa mishipa ya damu na hivyo kupelekea upungufu wa damu kwenye maeneo mumba iipojishikiza na kuamka kwa shinikizo la damu ili kusaidia kujitosheleza kwa kiwango cha damu inayohitajika kufika maeneo hayo.
Tafiti mpya zaidi zinaonyesha kuwa, tishu za kondo la nyuma huzalisha kemikali zenye jina la antiangiogenic factors kuitikia madhaifu katika kuta za mishipa ya damu na kupelekea pia ongezeko la shinikizo la damu
Hata hivyo wanasanyansi wanakubaliana kuwa, visababishi vingi huwa ni mchanganyiko wa sababu nyingi kama zilivyoeezewa hao juu.
Matibabu
Matibabu pekee ya kuondoa shinikizo la damu wakati wa ujauzito ni kujifungua, hata hivyo endapo hakuna haja ya kujifungua kwa wakati huo mama anaweza kutumia matibabu kinga au matibabu ya dawa kwa wenye tatizo tayari.
Matibabu ya Kinga
Kwa wanawake kuanzia ujauzito wa wiki 12 hadi 28 ambao wana kihatarishi kikuu kimoja au vidogo viwili na kuendelea wanapaswa kutumia Aspirin miligramu 81 kila siku
Vihatarishi vikuu ni pamoja na kuwa na historia ya shinikizo la juu la damu linaloelekea kifafa cha mimba(pre eclampsia), kuwa na kisukari aina ya 1 au 2, kuwa naugonjwa wa figo, magonjwa ya shambulio la kinga ya mwili, kuwa na ujauzito wa mapacha
Vihatarishi vidogo vinajumuisha, ujauzito wa kwanza, ujauzito wenye utofauti wa zaidi ya miaka 10, MBI zaidi ya 30, kuwa na uwezo mdogo wa kifedha, kuwa mwafrika, historia kwenye familia ya ndugu wa karibu wa damu moja kuwa na preeclampsia, ujauzito kwenye umri zaidi ya miaka 35, Historia ya mtoto ufia tumboni na ujauzito wa mwisho kuisha vibaya.
Matibabu dawa
Matibabu ya Shinikizo la juu la damu hutegemea kiwango cha shinikizo na mwitikio wa mama kwenye dawa. Hata hivyo matibabu yatahitajika endapo shinikizo la damu limekuwa juu na limeonekana kwa zaidi ya kipimo kimoja cha presha kufanyika kwa utofauti wa dakika 15. Baadhi ya dawa zinazotumika kudhibiti shinikizo la juu la damu ni pamoja na; labetolol, hydralazine, or Nifedipine, Clonidine, Magnesium na Methyldopa.
Dawa ambazo hazitakiwi tumika
Dawa jamii ya ACE inhibitors, angiotensin receptor bloka, mineralocorticoid receptor antagonists, na nitroprusside hazitakiwi tumika kwa sababu husababisha madhaifu ya kimaumbile kwa kijusi tumboni.
Dawa nitroprusside inaweza kutumika endapo tu shinikizo la damu halisikii dawa zingine
Kumbuka
Dawa hutumika endapo kuna uhaja, baadhi ya wanawake wenye shinikizo la damu la awali hawahitaji kutumia dawa, wale wenye shinikizo kabla ya ujauzito, endapo walikuwa wanatumia dawa, wanapaswa kuendelea kutumia dawa ambazo ni salama kipindi cha ujauzito.
Wasiliana siku zote na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya
Madhara
Madhara ya shinikizo la juu la damu ni pamoja na;
Kifafa cha mimba
Kuvilia kwa damu ndani ya kichwa
Kuferi kwa Ini
Kuharibiwa kwa chembe za damu
Matatizo ya kuganda kwa damu
Mapafu kuvia maji
Mtoto kutokukua tumboni
Maji kidogo kwenye chupa ya uzazi
Kuishiwa chembe nyekundu za damu
Kuchomoka kwa kondo la nyumakabla ya wakati wake
Kutokueleweka kwa viashiria vya uhai vya mtoto
Kuferi kwa figo
Soma zaidi kuhusu matatizo ya shinikizo la juu a damu na matibabuyake kwa kubofya linki hii https://www.ulyclinic.com/kifafa-cha-mimba-eclampsia
Rejea za majibu haya
Sarah C Fisher et al. Maternal antihypertensive medication use and selected birth defects in the National Birth Defects Prevention Study. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30260586/. Imechukuliwa 02.03.2021
Spiro L, et al. Management of Chronic and Gestational Hypertension of Pregnancy: A Guide for Primary Care Nurse Practitioners. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30258507/. Imechukuliwa 02.03.2021
Holm L, et al. Automated blood pressure self-measurement station compared to office blood pressure measurement for first trimester screening of pre-eclampsia. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30253712/. Imechukuliwa 02.03.2021
Miller MJ, et al. Implementation of a standardized nurse initiated protocol to manage severe hypertension in pregnancy. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30231657/. Imechukuliwa 02.03.2021
Dymara-Konopka W, et al. Preeclampsia - Current Management and Future Approach. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30255751/ Imechukuliwa 02.03.2021.
Gestational Hypertension and Preeclampsia: ACOG Practice Bulletin Summary, Number 222. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/32443077/. Imechukuliwa 02.03.2021.
ACOG Committee Opinion No. 743: Low-Dose Aspirin Use During Pregnancy. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/29939940/. Imechukuliwa 02.03.2021.
Smith GN, Pudwell J, Saade GR. Impact of the New American Hypertension Guidelines on the Prevalence of Postpartum Hypertension. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30170330/. Imechukuliwa 02.03.2021
Hauspurg A, et al. Aspirin Effect on Adverse Pregnancy Outcomes Associated With Stage 1 Hypertension in a High-Risk Cohort. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/29802215/. Imechukuliwa 02.03.2021