Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Glory, MD
ULY CLINIC
8 Juni 2025, 06:17:11
Nawezaje kutungisha mimba haraka?
Ili mwanaume aweze kutungisha mimba haraka, anapaswa kuhakikisha anafuata mbinu bora za kuongeza uwezo wake wa uzazi na kusaidia mwenza wake kuwa katika hali nzuri ya kupata mimba. Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia;

1. Kuongeza ubora na wingi wa mbegu
Kula lishe bora: Vyakula vyenye virutubisho kama vitamini C, D, E, zinki, na Omega-3 huimarisha afya ya mbegu.
Epuka vyakula vya mafuta mengi na sukari nyingi kwani vyakula hivi vinaweza kupunguza ubora wa mbegu.
Kunywa maji ya kutosha kwa kuwa mwili ukiwa na maji ya kutosha, uzalishaji wa mbegu huwa mzuri.
Epuka sigara, pombe, na dawa za kulevya kwa kuwa hupunguza uzalishaji na kasi ya mbegu.
Fanya mazoezi mara kwa mara kwa kuwa husaidia kuweka mwili katika hali nzuri na kuboresha mzunguko wa damu kwenye via vya uzazi.
Epuka joto kali kwenye sehemu za siri kwa kuepuka kufanya kazi na laptop juu ya mapaja, kuvaa nguo za kubana, au kuoga maji ya moto sana kwani joto hili linaweza kupunguza uzalishaji wa mbegu.
2. Kufanya tendo la ndoa Katika siku sahihi
Unapaswa kujua ni lini yai linatolewa (uovuleshaji) ambapo hutokea kati ya siku ya 12-16 katika mzunguko wa kawaida wa siku 28. Maelezo zaidi ya mzunguko huu na mingine imeelezewa kwenye linki hii
Shiriki tendo la ndoa mara kwa mara kila baada ya siku moja au mbili wakati wa uovuleshaji ili kuongeza nafasi ya kutungisha mimba.
Jitunze baada ya kushiriki tendo, hakikisha unamshauri mwenza wako kubaki amelala kwa dakika 15-30 baada ya tendo ili kusaidia mbegu kusafiri vizuri kuingia kwenye kizazi.
3. Kupima Afya ya Uzazi
Ikiwa jitihada zote hazifanikiwi ndani ya miezi 6-12, unaweza kupima kipimo cha mbegu hospitalini ili kuona ubora na wingi wa mbegu zako.
Rejea za mada hii:
Agarwal A, Mulgund A, Hamada A, Chyatte MR. A unique view on male infertility around the globe. Reprod Biol Endocrinol. 2015;13:37.
Salas-Huetos A, Bulló M, Salas-Salvadó J. Dietary patterns, foods and nutrients in male fertility parameters and fecundability: a systematic review of observational studies. Hum Reprod Update. 2017;23(4):371-389.
Esteves SC, Miyaoka R, Agarwal A. An update on the clinical assessment of the infertile male. Clinics (Sao Paulo). 2011;66(4):691-700.
World Health Organization. WHO Laboratory Manual for the Examination and Processing of Human Semen. 6th ed. Geneva: WHO Press; 2021.
Practice Committee of the American Society for Reproductive Medicine. Optimizing natural fertility: a committee opinion. Fertil Steril. 2017;107(1):52-58.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
