top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Amiba

Amiba ni nini?


Amoeba kwa jina jingine watu huita amiba, ni jamii ya vijidudu vidogo sana visivyoonekana kwa macho, ambavyo huishi katika maji na udongo, wametengenezwa kwa seli moja na huwa na uwezo wa kuabdilisha umbo lao kulingana na mazingira. Kuna amiba wa aina mbili wanaopatikana au kuathiri mfumo wa umeng’enyaji wa chakula kwa binadamu ambao ni Entamoeba histolytica- kisababishi cha ugonjwa wa amibiasisis na Entamoeba dispar, -rafiki wa faida kwa mwili kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula.


Magonjwa yanayosababishwa na Entamoeba histolytica


Entamoeba histolytica huzalisha vimeng’enya ambavyo vinaua seli ya binadamu iliyogusana na kimeng’enya hicho na pia hula chembe nyekundu za damu. Trophozoit (Vijidudu) wa Entamoeba histolytica huvamia kuta ya juu ndani ya tumbo na kusababisha kolaitiz ya amiba ambayo wengi hufahamu au huita ugonjwa wa amiba, ameba au amebiasis, amibiasis


Baadhi ya nyakati Entamoeba histolytica hutoboa ukuta wat umbo na kusafiri katika mishipa ya damu kwenda kwenye ini na hapo hupelekea ugonjwa wa jipu la amiba kwenye ini ambalo huwa lina vijidudu wachache na usaha.


Usaha huu hukua pasiko kuzuilika na ilipelekea kifo cha mtu katika miaka ambayo dawa hazikuwepo, ila kwa sasa hata kama usaha umekuwa kiasi gani unaweza kutibika kwa dozi moja tu ya dawa za antibayotiki.


Kumbuka


Amiba ni kimelea anayeweza kusababisha amibiasis ( kwa jina jingine kolaitiz ya amiba) au ugonjwa wa jipu la amiba kwenye ini.


Unapokuwa unamaambukizi kwenye tumbo ya amiba, tumia neno sahihi kwamba unaumwa ugonjwa wa amebiasis au amibiasis .


Soma zaidi kuhusu ugonjwa wa amibiasis dalili, tiba na dawa sehemu nyingine katika Makala za ULY CLINIC.


Rejea za mada hii


  1. Amoeba. https://www.britannica.com/science/amoeba-order. Imechukuliwa 26.06.2021

  2. Entamoeba Histolytica. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/12660071/. Imechukuliwa 26.06.2021

  3. Amebiasis. cdc.gov/parasites/amebiasis/general-info.html. Imechukuliwa 26.06.2021

  4. Pearson, R. D.Amebiasis. merckmanuals.com/home/infections/parasitic-infections/amebiasis. Imechukuliwa 26.06.2021

211 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page