top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kukosa uzingizi| ULY CLINIC

Jamani mimi naitwa.......... nilipata mimba ila wakati wa mimba nilikua na lala vizuri sana ila baada ya kujifungua sipati kabisa usingizi na wala sisikii usingiz sijui hili ni tatizo gani na je linatibika

5 Views

Pole sana ..... kwa tatizo hili. Kukosa usingizi (insomnia) ni tatizo endelevu  linalosababisha mtu kushindwa kuanza kusinzia, kutodumu kwenye usingizi ama vyote viwili licha ya kupata fursa ya kulala ipasavyo.  Kwa kukosa usingizi, mtu huyu kwa kawaida huamka hajihisi kuwa mpya , hali hii inasababisha kupunguza uwezo wa kufanya kazi wakati wa mchana.kukosa usingizi hakumalizi nguvu tu na hali yako, bali hudhuru afya na ubora wa maisha. Soma zaidi kwa kubonyeza hapa au bonyeza hapa kusoma kuhusu matibabu ya nyumbani ya kukosa uzingizi.


Wasiliana na daktari wako ili atambue ni nini shida yako baada ya kusoma makala hii.


Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kutumia namba za simu chini ya tovuti hii.

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page