Wakati gani wa kunywa pombe mara baada ya kumaliza dozi ya dawa
Habari daktari, Naitwa Mr. X ni mwandishi wa habari, Naomba kufahamu ni muda gani kitaalamu mtu anaruhusiwa kutumia pombe baada ya kumaliza dozi ya typhoid au malaria?
832 Views
Habari daktari, Naitwa Mr. X ni mwandishi wa habari, Naomba kufahamu ni muda gani kitaalamu mtu anaruhusiwa kutumia pombe baada ya kumaliza dozi ya typhoid au malaria?
Asante kwa swali ndugu X.
Pata majibu kwenye kipeperushi ndani ya boksi la dawa
Majibu ya swali hili yanapatikana kwenye kipeperushi maalumu kinachowekwa na mtengeneza dawa ndani ya boksi la dawa. Kipeperushi hii hutoa ushauri endapo dawa inaruhusiwa kutumika na pombe au la, endapo hakipo, muulize mtaalamu wa dawa aliyekuuzia dawa hiyo.
Majibu ya swali
Muda gani upite toka umemaliza dawa ndipo unywe pombe inategemea dawa na dawa na pia umri wa mtu. Hata hivyo kiwango cha dawa nyingi huwa kimepungua kwa kiasi kikubwa au kupotea kabisa kwenye damu baada ya masaa 72 (siku tatu) na wakati huo mtu anaweza kuanza kutumia pombe.
Kumbuku ni vema kusoma zaidi kwenye kipeperushi cha dawa kinachopatikana ndani ya boksi la dawa.
Kufahamu zaidi kuhusu dawa gani ambazo hazitakiwi tumika na pombe bofya hapa
Na
Kufahamu muda gani upite ili uweze kutumia pombe au kipindi salama cha kutumia pombe na dawa bofya hapa
ULY CLINIC inapenda na kuthamini afya yako, hii ndo maana haisiti kujibu maswali yote yanayoulizwa na wateja.
Je unaswali la kiafya na unahitaji majibu ya kitaalamu?
Kuuliza maswali tumia namba za simu chini ya tovuti hii au email ya info@ulyclinic.com utapatiwa majibu bure.