top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

je, ni vyakula vipi unatakiwa utumie iwapo umegundulika acid inapanda kooni?

Kucheua tindikali ( acid kupanda kooni) ni ugonjwa unaotokea sana. Baadhi ya watu hata hivyo hupata tatizo la tumbo kujaa, kubeua mara kadhaa baada ya kula.

Chakula huchukua nafasi kubwa katika matibabu ya hali hizi pamoja na ugonjwa wa kucheua tindikali.


Makala hii imeelezea kuhusu vyakula vinavyochochea au kusababisha kucheua tindikali na kiungulia na vile ambavyo vinapunguza au kutibu tatizo hili.


Vyakula vinavyosababisha kiungulia/kucheua tindikali

Vyakula hivi hufahamika kulegeza koki ya chini ya umio na hivyo kusababisha kucheua na matatizo mengine ya tumbo;


  • Vyakula vya kukaanga

  • Piza

  • Chipsi jna vitafunwwa vingine vyenye mafuta kwa wingi

  • Pilipili na chili sosi

  • Nyama yenye mafuta pamoja na soseji

  • Siagi

  • Sosi ya njanya

  • Nyanya

  • Matunda jamii ya citrus kama limao, ndimu

  • Siki ya tufaa

  • Chocolate

  • Minti hupatikana kwenye bazoka (bablishi) na baadhi ya dawa ya mswaki n.k

  • Vinywaji vilivyotiwa carbon kama vile soda n.k

  • Nanasi

  • Machungwa

  • Vyakula vyenye viungo kwa wingi kama vitunguu, tangawizi na pilipili

  • Kahawa

  • Pombe


Vyakula vinavyozuia kiungulia na kucheua tindikali

Kuna aina kadhaa ya makundi ya vyakula vinavyozuia kiungulia, vyakula hivi huwa na ualkali kwa wingi. Baadhi yake ni;


  • Nafaka zisizokobolewa kama mchele wa brauni, mtama na uwele

  • Vyakula jamii ya mizizi kama vile viazi vitamu, karoti na kiazi kitamu (biti)

  • Mboga za majani kama vile asparagazi, brokoli na maharagwe ya kijani au saladi yenye mbogha za majani kwa wingi

  • Ndizi

  • Boga

  • Karanga

  • Funnel

  • Ute wa yai

  • Tango

  • Tikiti maji

  • Chai yenye tangawizi kwa kiasi kidogo

  • Spinachi

  • Maziwa ya mgando yenye mafuta kidogo

  • Nyama isiyo na mafuta


Mambo mengine ya kuzingatia


  • Epuka kula mlo mzito, kula milo midogo midogo ili kuzuia tumbo kujaa na kulegea kwa koki inayozuia kucheua chakula.

  • Epuka kula unapokaribia wakati wa kulala haswa ndani ya masaa 3 hadi 4 kabla ya kulala

  • Tumia dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali kama utakavyoshauriwa na daktari wako

  • Kuwa na uzito wa kiafya

  • Acha kutumia pombe

  • Acha kuvuta sigara

  • Usile haraka haraka

  • Kaa wima angalau masaa mawili baada ya kula

  • Usivae nguo za kubana

  • Tumia mto wakati wa kulala kufanya kichwa kiwe juu kidogo ili kuzuia kucheua


Rejea za mada hii;


  1. John hopkins medicine. GERD Diet: Foods That Help with Acid Reflux (Heartburn). https://www.hopkinsmedicine.org/health/wellness-and-prevention/gerd-diet-foods-that-help-with-acid-reflux-heartburn

  2. Acid reflux (GER and GERD) in adults. (n.d.). niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/acid-reflux-ger-gerd-adults

  3. Allergens and allergic asthma. (2015). aafa.org/page/allergic-asthma.aspx

  4. Diet changes for GERD. (2021). aboutgerd.org/diet-lifestyle-changes/diet-changes-for-gerd.html

  5. Kahrilas P, et al. (2017). Emerging dilemmas in the diagnosis and management of gastroesophageal reflux disease. 10.12688/f1000research.11918.1

  6. Kaur K, et al. (2015). Chapter 6: Medicinal benefits of ginger in various gastrointestinal ailments: Use in geriatric conditions. sciencedirect.com/science/article/pii/B9780124186804000063

  7. Morozov, S, et al. (2018). Fiber-enriched diet helps to control symptoms and improves esophageal motility in patients with non-erosive gastroesophageal reflux disease. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5989243/

1803 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page