top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Matapishi mekundu

Kutapika damu husababisha kupata mataapishi yenye rangi nyekundu au nyeusi endapo damu imekaa kwa muda mrefu tumboni.


Kutapika matapishi mengi yenye rangi nyekundu au meusi huitwa kitiba ‘hematemesis’


Visababishi vya kutapika damu kwa watoto ni;


  • Kutostahimili chakula

  • Damu kutoka kwenye majeraha ndani ya kinywa

  • Madhaifu ya kuganda kwa damu

  • Madhaifu ya kuzaliwa kwenye mfumo wa mumeng’enyaji chakula au mishipa ya damu


Visababishi vya kutapika damu kwa watu wazima ni;


  • Majeraha kwenye kinywa, koo, fizi kutokana na kukohoa n.k

  • Vidonda vya tumbo au vidonda katika sehemu yoyote ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula

  • Ugonjwa wa amilaidosis

  • Kuferi kwa Ini ambako huonekana na dalili zingine kama manjano n.k

  • Majeraha ya umio kutokana kutapika kwa nguvu au sana


Wakati gani unapaswa kuwa na hofu unapotapika?


Endapo unatapika matapishi mekundu yanayoambatana na dalili zifuatazo unapaswa kutilia mashaka na kutafuta msaada wa daktari;


  • Kizunguzungu

  • Kupumua kwa shinda

  • Kutapika nyongo kwa muda mrefu

  • Kutapika zaidi ya masaa 48 bila kupata nafuu

  • Kutapika kila kitu

  • Maumivu makali ya tumbo nay a ghafla

  • Kuwa na kisukari

  • Maumivu makali ya kifua

  • Kutapika mara kwa mara katika mwaka

  • Matapishi kuwa meusi au rangi ya unga wa kahawa

  • Maumivu makali ya kichwa na homa

  • Kuishiwa nguvu au kupata uchovu mkali

  • Kupata kizunguzungu au kuzimia


Huduma ya kwanza kwa mtu anayetapika sana;


Hatua ya muhimu kuchukua endapo unatapika sana ni kufika hospitali ili kupatiwa matibabu kw akutundikiwa dripu, hii itasaidia rejesha kiwango cha madini na maji ulichopoteza.


Kama unatapika kwa kiasi na unaweza kunywa maji, fanya iwezekanavyo kunywa maji kiasi kidogo sana lakini mara kwa mara. Ukipata maji ya Oral au wengine huita ORS na hutumika kwa watoto wanaoharisha itasaidia kuwa kama huduma ya kwanza. Kengo ni kurejesha kiwango ulichopoteza kwa kutapika na kuzuia kupata shoku kutokana na kuishiwa maji mwilini.


Zuia kutumia vitu vinavyokuletea kichefuchefu kama vinywaji nyenye mafuta, sukari na viungo kwa wingi na vingine ambavyo vinaamsha kuchefuchefu chako.


Rejea za mada hii;


  1. Vomiting in adults. https://www.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021

  2. Catiele Antunes, et al. Upper Gastrointestinal Bleeding. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470300/#: Imechukuliwa 28.06.2021

  3. I.Dodd Wilson. Chapter 85Hematemesis, Melena, and Hematochezia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK411/. Imechukuliwa 28.06.2021

  4. Amyloidosis. my.clevelandclinic.org/health/diseases/15718-amyloidosis. Imechukuliwa 28.06.2021

  5. Cyclic vomiting syndrome. niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/cyclic-vomiting-syndrome. Imechukuliwa 28.06.2021

  6. Lamps LW, et al.Fungal infections of the gastrointestinal tract in the immunocompromised host: An update. DOI: 10.1097/PAP.0000000000000016. Imechukuliwa 28.06.2021

  7. Mayo Clinic Staff. Acute liver failure. mayoclinic.org/diseases-conditions/acute-liver-failure/symptoms-causes/syc-20352863. Imechukuliwa 28.06.2021

  8. Mayo Clinic Staff. Viral gastroenteritis (stomach flu). https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/viral-gastroenteritis/symptoms-causes/syc-20378847. Imechukuliwa 28.06.2021

  9. Mayo Clinic Staff.Food poisoning. mayoclinic.org/diseases-conditions/food-poisoning/symptoms-causes/syc-20356230. Imechukuliwa 28.06.2021

  10. Mayo Clinic Staff.Gastritis.mayoclinic.org/diseases-conditions/gastritis/symptoms-causes/syc-20355807. Imechukuliwa 28.06.2021

  11. Mayo Clinic Staff.Gastroesophageal reflux disease (GERD). mayoclinic.org/diseases-conditions/gerd/symptoms-causes/syc-20361940. Imechukuliwa 28.06.2021

  12. Mayo Clinic Staff.Intestinal obstruction. mayoclinic.org/diseases-conditions/intestinal-obstruction/symptoms-causes/syc-20351460. Imechukuliwa 28.06.2021

  13. Mayo Clinic Staff.Nausea and vomiting. mayoclinic.org/symptoms/nausea/basics/definition/sym-20050736. Imechukuliwa 28.06.2021

  14. Mayo Clinic Staff.Vomiting blood. mayoclinic.org/symptoms/vomiting-blood/basics/definition/sym-20050732

  15. Nausea and vomiting in adults. nhs.uk/conditions/nausea-and-vomiting-in-adults/. Imechukuliwa 28.06.2021

  16. Nausea and vomiting. my.clevelandclinic.org/health/symptoms/8106-nausea--vomiting. Imechukuliwa 28.06.2021

  17. Vomit looks like coffee grounds after drinking alcohol. goaskalice.columbia.edu/answered-questions/vomit-looks-coffee-grounds-after-drinking-alcohol. Imechukuliwa 28.06.2021

  18. Vomiting in adults. (2018). nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021

44 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page