top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kuonekana kwa HIV kwenye kipimo

Swali la msingi na 01


Habari doctor, Je, mtu anaweza kuishi na maambukiz ya HIV ndani ya miezi sita na kwenye kipimo asioneshe ana maambukizi?


Majibu ya Kipimo cha HIV

Majibu ya daktari ya swali na 01

Ikiwa mtu amepima baada ya miezi sita na hajashiriki ngono tena baada ya tukio la hatari, na bado hana maambukizi, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba hana HIV. Kipindi cha dirisha la matazamio huwa kati ya wiki 2 hadi miezi 3 kwa vipimo vya kisasa, hivyo baada ya miezi sita, majibu ya vipimo vinapaswa kuwa sahihi na kuaminiwa. Ikiwa mtu alikuwa ameambukizwa, kipimo kingeonyesha matokeo chanya. Ikiwa bado una wasiwasi, unaweza kurudia kipimo.


Swali kutoka kwa daktari na 01

Je, inamaanisha kuwa mtu huyu hajashiriki ngono bila kinga kwa miezi sita mfululizo pia?


Majibu ya muulizaji ya swali la daktari na 01

Kashiriki pengine mwez wa pil akapat baadhi ya dalili ila amekaa miez sita anaenda kupima yupo negative akaakaa tena miezi 3 ni negative.


Majibu ya Daktari kutokana na majibu ya muulizaji

Kila mara mtu anaposhiriki ngono bila kinga, anapaswa kupima katika kipindi cha baada ya dilisha la matazamio. Kama ilivyoelezewa hapo awali, vipimo vya sasa vinachukua muda wa wiki 2 hadi miezi 3 kuonyesha majibu sahihi. Ikitegemea aina ya kipimo utakachotumia, unaweza kupima baada ya mwezi mmoja hadi miezi 3 tangu umeshiriki ngono mara ya mwisho.


Mambo ya kuzingatia wakati unasubiri kupita kwa dilisha la matazamio

Katika kipindi cha kusubiria majibu sahihi ya kipimo ili kufahamu kama kushiriki kwako mara ya mwisho kumepelekea maambukizi au la, unapaswa kutumia kinga, la sivyo hutapata majibu sahihi kwa kuwa kila unaposhiriki ngono bila kinga utapaswa kusubiria kipindi cha dilisha la matazamio kupita.


Rejea za majadiliano haya:

  1. ULY CLINIC. Window period. https://www.ulyclinic.com/vidokezo-vya-kiafya/window-period-ya-vipimo-vya-vvu. Imechukuliwa 31.03.2025

20 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page