top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kumwogesha kichanga

Unaweza kupata shida kama ni mara ya kwanza kumuogesha kichanga kwa sababu ya huwa mdogo na mwenye kuteleza, hali inayoweza kupelekea kumdondosha mtoto. Utakuwa mzoefu na kupata ujuzi kadili siku zinavyoenda na utaona ni jambo la kawaida.


Nini maana ya kichanga?


Kichanga ni mtoto mwenye chini ya umri chini ya mwezi mmoja.


Kichanga anatakiwa kuoga muda gani baada ya kuzaliwa?


Inashauriwa kuchelewa kumwogesha kichanga angalau masaa 24 baada ya kuzaliwa. Kama haiwezekani kusubiria masaa 24 basi angalau kusubiria masaa 6 toka amezaliwa.


Kwanini kusubiria hadi masaa 24 kupita ndipo kumwogesha kichanga?


Kumwogesha mtoto mara anapozaliwa kunaongeza hatari ya;

  • Kushuka kwa kiwango cha sukari na joto la mwili

  • Kuepuka mtoto kupata baridi na kushuka kwa sukari kutokana na msongo mwilini

  • Kuzuia muungano wa mama na mtoto pamoja na kuathiri uzalishaji wa mziwa

  • Kukauka kwa ngozi ya mtoto kutokana na kuondoa poda asili ambayo inatunza ngozi na kupambana na maambukizi ya ngozi


Ni mara ngapi kichanga anatakiwa kuoga?


Wengi hudhani ni lazima kumwogesha kichanga kila siku, hii si kweli kwani mtoto anaweza kuoga mara 3 tu kwa wiki na bado akawa msafi. Kutomwogesha kichanga mara kwa mara kutafanya kitovu chake kiwe kikavu na kudondoka haraka na pia kuzuia kukauka kwa ngozi ya mtoto kutokana na kuoga mara kwa mara.


Kama humwogeshi mara kwa mara nini unatakiwakuzingatia?


Kama unamwogesha kichanga mara 3 au 4 kwa wiki, hakikisha unafanya mambo yafuatayo;

  • Kubadilisha pampasi au nepi mara anapojisaidia haja ndogo au kubwa

  • Msafishe usoni, shingoni na maeneo chini ya kitovu, kwa kutumia kitambaa kikavu kilichocholowekwa kwenye maji ya uvuguvugu ili awe msafi

  • Mvalishe pampasi au nepi safi baada ya kumsafisha


Ni wakati gani wa kumwogesha kichanga


Unaweza kumwogesha kichanga muda wowote ule utakaochagua mfano wakati unataka kumlaza au akiwa anaamka au baada ya kunyonya. Licha ya kumwogesha muda wowote, subiri muda wa wa dakika 10 hadi 20 toka umemnyonyesha ili chakula kitulie tumboni.


Njia gani nzuri ya kumwogesha kichanga?




Njia nzuri ya kumwogesha kichanga ni kwa kumfuta kwa kitambaa kilichokamuliwa baada ya kuchovywa kwenye maji vuguvugu yenye sabuni ya kumuogeshea mtoto. Njia hii ni zuri kutumika kuanzia mtoto anapozaliwa mpaka pale kitovu kitakapoanguka.


Vitu gani utahitaji ili kumwogesha mtoto kwa kumfuta


Utahitaji kuwa na;


  • Eneo tambalale lenye ujoto kama vile meza ya kubadilishia nguo ambayo imetandikwa blanketi laini n.k

  • Taulo au kitenge safi cha kumfunga mtoto baada ya kuoga

  • Mkono mmoja wenye uhuru au kuwa na mtu wa pili atakayekusaidia

  • Beseni la kuwekea maji

  • Maji ya uvuguvugu, hakikisha umeweka mikono yako ili kufahamu kama ni ya uvuguvugu au ya moto ili uepuke kumuunguza mtoto

  • Sabuni, mafuta ya kumpaka mtoto, nepi na nguo ya kubadilisha baada ya kuoga yenye kofia


Namna ya kumwogesha kichanga


Mvue nguo mtoto kisha mfunike kwa taulo na kumlaza kwenye eneo tambalale ambalo umeliandaa


Lowanisha taulo ya kumwogeshea kichanga kwenye maji ya uvuguvugu kisha kamua na kumfuta maeneo ya usoni. Futa kwenye kila kona ya kope za macho kutoka ndani kwenda nje.


Fanya hivyo hivyo kumfuta sehemu za kiwiliwili chake huku ukukimbuka maeneo muhimu yenye mikunjo kama kwapani, shingoni, nyuma ya sikio, maeneo yake ya siri na nepi inapopita na katikati ya vidole. Tumia maji yasiyotiwa yasiyotiwa sabuni au yenye sabuni za kuleta unyevu kwenye ngozi.


Ni wakati gani mtoto ataoga kwa kuzamishwa kwenye maji?


Unaweza kumwogesha mtoto kwa kutumia maji wiki mbili baada ya kitovu kukatika. Tumia beseni au sinki la kuogea kuweka kiasi kidogo cha maji ya uvuguvugu kiasi kwamba masikio ya mtoto yasiguswe na maji kama akilala chali kwenye maji hayo. Usimwache mtoto mwenyewe kwenye beseni lenye maji kwani si salama.


Unaweza kutumia maji mengi zaidi?


Ndio unaweza kutumia maji mengi zaidi endapo utakuwa karibu na mtoto, tafiti zinaonyesha kuwa kutumia maji ya kuweza kuzamisha mabega ya mtoto kwenye maji husaidia kutuliza mtoto na kuzuia kupotea kwa joto la mwili.


Maji yawe na joto kiasi gani?


Kama una kipima joto unaweza kukitumia kupooza maji ya moto ili yafikie nyuzi 40 za selishazi. Kama huna kipima joto tumia mikono yako kupima joto la maji, lengo ni kutumia maji ya uvuguvugu na si ya moto. Mwogeshe mtoto kwenye chumba ambacho kina joto ili kuepuka kutetemeka baada ya kuoga.


Unaweza kumuogesha mtoto nywele zake


Ndio!


Kama unahisi mwanao anahitaji kuoshwa nywele zake, safisha taratib kwa kutumia sabuni kidogo ya kusafisha nywele za mtoto kisha futa na kitambaa chenye unyevu au tumia maji, hakikishamaji hayagusi kiwiliwili au kuingia machoni


Baada ya mtoto kuoga anaweza kupakwa mafuta?


Vichanga wengi huwa hawahitaji kupaka mafuta baada ya kuoga isipokuwa endapo ngozi ni kavu. Kama ngozi imekuwa kavu, mpake mafuta kidogo ya kuleta unyevu kwenye ngozi na mkande wakati unampaka ili ajihisi vema. Endapo ngozi ya mtoto inakauka sana, inaweza kuwa unamuogesha mara kwa mara au kutumia sabuni zinazokausha ngozi.


Rejea za mada hii;


  1. Shelov SP, et al. Basic infant care. In: Caring for Your Baby and Young Child: Birth to Age 5. 5th ed. New York, N.Y.: Bantam Books; 2014.

  2. Ness MJ, et al. Neonatal skin care: A concise review. International Journal of Dermatology. 2013;52:14.

  3. Jana LA, et al. Baby bath basics. In: Heading Home With Your Newborn: From Birth to Reality. 3rd ed. Elk Grove Village, Ill.: American Academy of Pediatrics; 2015.

  4. Umbilical Cord Care. https://americanpregnancy.org/healthy-pregnancy/first-year-of-life/umbilical-cord/. Imechukuliwa 17.07.2021

  5. Bathing Your Baby. https://www.healthychildren.org/English/ages-stages/baby/bathing-skin-care/Pages/Bathing-Your-Newborn.aspx. Imechukuliwa 17.07.2021

785 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page