top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Dalili za amoeba

Dalili za amoeba

Amoeba au amoebiasis ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea Entamoeba histolytica. Maambukizi haya mara nyingi huathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, hasa utumbo mpana.


Dalili za Amoeba

Dalili za amoeba zimegawanyika katika makundi mbalimbali zikiwa zinaashiria hatua ya ugonjwa, ambapo zinaweza kuwa nyepesi, za wastani, au kali, kulingana na kiwango cha maambukizi.


Dalili nyepesi za amoeba (katika tumbo)

  • Kuhara kunakoweza kuambatana na kuhara damu au ute

  • Maumivu ya tumbo

  • Tumbo kujaa gesi

  • Kuhisi kichefuchefu

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kupungua uzito bila sababu ya msingi

  • Homa nyepesi


Dalili kali za amoeba wa tumbo (katika tumbo)

  • Kuhara damu mara kwa mara

  • Maumivu makali ya tumbo

  • Homa kali

  • Uchovu mkubwa kutokana

  • Upotevu wa maji mwilini


Dalili za amoeba katika Ini

Amoeba akisambaa kwenye ini husababisha ini kutunga usaha, dalili zake ni pamoja na;

  • Homa kali inayoambatana na jasho

  • Maumivu makali upande wa juu kulia mwa tumbo (eneo la ini)

  • Kupungua uzito haraka

  • Kuhisi uchovu

  • Kudhoofika mwili


Wakati gani wa kumwona daktari haraka unapokuwa na dalili za amoeba?

Unapaswa kutafuta matibabu ya haraka ikiwa unakumbwa na dalili kali za amoeba kama vile;


Dalili za Upungufu Mkubwa wa maji mwilini

Mfano wa dalili ni kama

  • Kuhara mfululizo (zaidi ya mara 6 kwa siku)

  • Kutapika kupita kiasi, kiasi cha kushindwa kunywa maji

  • Kiu kali, mdomo mkavu, macho yaliyodidimia

  • Kizunguzungu, kuchanganyikiwa, au kuzimia


Unapata kinyesi chenye damu au maumivu makali ya tumbo

Dalili hii inaweza kuambatana pia na;

  • Kuhara damu au kinyesi chenye ute mwingi

  • Maumivu makali ya tumbo au tumbo kuwa na ugumu

  • Tumbo kuvimba au kuhisi limejaa sana


Unapata dalili za maambukizi ya Ini

Dalili hizo ni kama vile;

  • Maumivu makali upande wa juu kulia wa tumbo

  • Homa kali (zaidi ya 38.5°C au 101°F)

  • Kupungua uzito kwa kasi na uchovu mwingi

  • Njano kwenye ngozi na macho


Unapata dalili za maambukizi yanayoenea kwenye mwili

Dalili hizo ni kama vile;

  • Homa kali inayoambatana na kutetemeka na jasho

  • Kupumua kwa shida au maumivu ya kifua (ikiathiri mapafu)

  • Tumbo kuvimba na maumivu makali (hatari ya ini kupasuka)


Una dalili za kawaida lakini upo kwenye makundi maalumu

Makundi yaliyo katika hatari zaidi ni kama; 

  • Wajawazito

  • Watoto wachanga na wadogo

  • Wazee

  • Watu wenye kinga dhaifu (wenye HIV, kisukari, saratani, n.k.)


Vipimo vya ugonjwa wa amoeba

Ili kuthibitisha maambukizi ya Entamoeba histolytica (amoeba), madaktari hutumia mchanganyiko wa dalili za mgonjwa, vipimo vya maabara, na historia ya mgonjwa.


Historia ya Mgonjwa na dalili za kitiba

  • Kuhara kinyesi chenye damu au ute

  • Maumivu ya tumbo (hasa eneo la chini la tumbo au upande wa kulia juu ikiwa ini limeathirika)

  • Homa na uchovu ikiwa maambukizi ni makali

  • Kupungua uzito bila sababu ya msingi

  • Kichefuchefu au kutapika

Vipimo vya Maabara kwa uchunguzi wa Kinyesi

  • Hadubini ya wet mount– Kuangalia vimelea vya Entamoeba histolytica chini ya darubini

  • Kipimo cha antijen kwenye kinyesi(EIA/ELISA) – Kugundua protini za amoeba kwa usahihi zaidi

  • Kipimo PCR – Hutumika kutofautisha E. histolytica na aina zisizo hatari kama E. dispar


Vipimo vya Maabara kwa uchunguzi wa damu

  • Kipimo ELISA – Hutambua kingamwili dhidi ya E. histolytica, hasa kwa maambukizi ya muda mrefu

  • Indirect hemagglutination test (IHA) – Hutumika kwa maambukizi sugu


Vipimo vya picha

Ikiwa kuna dalili za maambukizi katika ini (amoebic liver abscess), vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika:

  • Ultrasound ya tumbo – Kugundua usaha kwenye ini

  • CT Scan / MRI – Kuangalia uvimbe au vidonda kwenye ini


Vipimo vya jumla

Vipimo hivi hufanyika ili kuangalia hali ya mwili na kusaidia katika maamuzi ya tiba;

  • Full Blood Count (FBC) – Inaweza kuonyesha ongezeko la seli nyeupe za damu (leukosaitosis) ikiwa kuna jipu la amoeba

  • Liver function tests (LFTs) – Ikiwa ini limeathirika, vipimo vya ini vinaweza kuonyesha mabadiliko katika vimeng'enya vya ini na utendaji kazi wake.


Vigezo vya uhakika wa ugonjwa wa Amoeba

Vigezo vifuatavyo vikiwepo, utathibitika kuwa una ugonjwa wa amoeba;

  • Kimelea Entamoeba histolytica ameonekana katika kinyesi au kinyongo

  • Dalili na historia inaendana na maambukizi ya amoeba

  • Ushahidi wa jipu la amoeba kwenye ini kwa kipimo cha Ct scan au ultrasound

  • Ongezeko la kingamwili dhidi ya kimelea wa amoeba katika vipimo vya damu


Matibabu ya Amoeba

Madaktari hutibu amoeba kwa kutumia dawa kama:

  • Metronidazole au Tinidazole – Kuua vimelea vya amoeba

  • Paromomycin – Kuondoa mabaki ya vimelea kwenye utumbo

  • Dawa za kutibu dalili – Kama vile ORS kwa kuzuia upungufu wa maji mwilini


Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Amoeba

  • Kunywa maji safi na salama

  • Kuosha matunda na mboga vizuri

  • Kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni

  • Epuka kula chakula cha mitaani ambacho si safi



Kama una dalili zinazodumu kwa muda mrefu au zinaongezeka, ni muhimu kutafuta matibabu haraka.


Rejea za mada hii;

  1. Saidin S, et al. Update on laboratory diagnosis of amoebiasis. Eur J Clin Microbiol Infect Dis. 2019 Jan;38(1):15-38.

  2. Kumanan T, et al. Amoebic Liver Abscess and Indigenous Alcoholic Beverages in the Tropics. J Trop Med. 2018;2018:6901751.

  3. Shirley DT, et al Review of the Global Burden, New Diagnostics, and Current Therapeutics for Amebiasis. Open Forum Infect Dis. 2018 Jul;5(7):ofy161.

  4. Fleming R, et al. Clinical manifestations and endoscopic findings of amebic colitis in a United States-Mexico border city: a case series. BMC Res Notes. 2015 Dec 14;8:781.

  5. Guevara Á, et al. Use of Real-Time Polymerase Chain Reaction to Differentiate between Pathogenic Entamoeba histolytica and the Nonpathogenic Entamoeba dispar in Ecuador. Am J Trop Med Hyg. 2019 Jan;100(1):81-82.

  6. Chacín-Bonilla L. [An update on amebiasis]. Rev Med Chil. 2013 May;141(5):609-15.

  7. González-Alcaide G, et al. Areas of research and clinical approaches to the study of liver abscess. World J Gastroenterol. 2017 Jan 14;23(2):357-365.

  8. Burchard GD. [Treatment of diseases acquired abroad]. Internist (Berl). 2014 Sep;55(9):1100, 1012.

  9. Anwar A, et al. Combating Acanthamoeba spp. cysts: what are the options? Parasit Vectors. 2018 Jan 09;11(1):26.

73 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page