top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

mimi nina tatizo la kisukari, je ni mazoezi gani nifanye?

Hili ni swali ambalo wagonjwa wa kisukari wamekuwa wakiniuliza hospitali, majibu yake ni mengi lakini naweza kulijibu kama ifuatavyo

kwanza kabisa wagonjwa wakisukari naomba watambue kwamba Kuzingatia mazoezi tu na chakula kunasaidia kudhibiti kupanda kwa sukari, inaweza kufika kipindi usihitaji kutumia dawa kwa sababu ya sukari kuwa katika kiwango kinachotakiwa kwa njia ya mazoezi na chakula.


Nirudi kwenye swali la msingi, yapo mazoezi ya aina kadhaa ya kufanya kwa mgonjwa wa kisukari, mazoezi haya hutegemea hali ya mtu lakini kwa ujumla yanahusisha yale ya aerobic, mazoezi ya ukinzani na mazoezi ya mjongeo. Kila ainaya mazoezi ina faida yake katika mwili wa mgonjwa wa kisukari. Mgonjwa wa kisukari anatakiwa kufanya mazoezi angalau kwa jumla ya dakika 150 kwa wiki, mazoezi haya yakiwa yale yangazi ya kati. yaani simepesi wala si magumu. Maelezo zaidi kuhusu aina hizi za mazoezi zimeelezewa katika mtandao huu nisingependa kurudia. bonyeza hapa kusoma


31 Views
ngowinovathi
Apr 14

je inahusiana nn clinic hii

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page