top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Utajuaje kama umepona gono?

Kwa kawaida utafahamu kuwa umepona gono kama dalili ulizokuwa nazo zimepotea. Hapa ifahamike kuwa ni kupotea kwa dalili tu bali si kupotea kwa madhara yanayosababishwa na gono isiyotibiwa kwa wakati ambayo baadhi yake huwa ya kudumu.


Dalili za gono ambazo zitapotea kama umepona gono

  • Kama unatokwa na usaha, utaacha kutoka usaha

  • Kama ulikuwa ukipata maumivu wakati wa kukojoa, yatakuwa yakipungua kwa jinsi muda unavyoenda na kuisha kabisa

  • Kama ulikuwa unapata maumivu wakati wa kujamiana, yataisha kwa jinsi muda unavyoenda

  • Kama ulikuwa na maumivu wenye korodani, yataisha kwa jinsi muda unavyoenda


Madhara ya gono kwa mwanaume yanayoendelea kwa aliyepona gono lakini hakupata tiba mapema

Baadhi ya madhara au dalili zinazoweza kuendelea ni"

  • Makovu kwenye mrija urethra- Yanaweza kuendeleza dalili za maumivu, mkojo kutotoka vema n.k

  • Kusinyaa kwa mrija wa urethra- Inaweza pelekea pia kutoboka kwa mrija wa mkojo

  • Maumivu sugu ya mrija wa urethra

  • Utasa


Madhara ya gono kwa mwanamke yanayoendelea kwa aliyepona gono lakini hakupata tiba mapema


Baadhi ya madhara au dalili zinazoweza kuendelea ni"

  • Makovu kwenye mrija wa falopia- makovu makubwa huendelea na huwa na athari katika uzazi

  • Kusinyaa kwa mrija wa falopia- Huwa na athari katika kupitisha mayai ya uzazi

  • Maumivu sugu ya tumbo la chini kutokana na makovu endelevu ndani

  • Utasa

Wapi utapata maelezo zaidi kuhusu kupona gono?

Unaweza kupata maelezo zaidi katika makala zifuatazo


Rejea za mada hii:


  1. ULY CLINIC- Madhara ya gono. https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/madhara-ya-gono. Imechukuliwa 03.10.2024

  2. CDC fact sheet (detailed version). Gonorrhea. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/std/gonorrhea/stdfact-gonorrhea.htm. Imechukuliwa 28.05.20222. Ghanem KG. Clinical manifestations and diagnosis of Neisseria gonorrhoeae infection in adults and adolescents. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.05.20223.

  3. Office on Women's Health. Gonorrhea. . https://www.womenshealth.gov/a-z-topics/gonorrhea. Imechukuliwa 28.05.20224. Merck Manual Professional Version. Gonorrhea. https://www.merckmanuals.com/professional/infectious-diseases/sexually-transmitted-diseases-stds/gonorrhea. Imechukuliwa 28.05.20225.

  4. Chlamydia, gonorrhea, and nongonococcal urethritis. Mayo Clinic; 2019.Speer ME. Gonococcal infection in the newborn. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.05.2022

187 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page